Surah Araf aya 169 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ وَرِثُوا الْكِتَابَ يَأْخُذُونَ عَرَضَ هَٰذَا الْأَدْنَىٰ وَيَقُولُونَ سَيُغْفَرُ لَنَا وَإِن يَأْتِهِمْ عَرَضٌ مِّثْلُهُ يَأْخُذُوهُ ۚ أَلَمْ يُؤْخَذْ عَلَيْهِم مِّيثَاقُ الْكِتَابِ أَن لَّا يَقُولُوا عَلَى اللَّهِ إِلَّا الْحَقَّ وَدَرَسُوا مَا فِيهِ ۗ وَالدَّارُ الْآخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ﴾
[ الأعراف: 169]
Na wakafuatia baada yao kizazi kibaya walio rithi Kitabu. Wakashika anasa za haya maisha duni, na wakasema: Tutasamehewa! Na ikiwajia tena anasa kama hiyo wataishika pia. Je, hawakufanyiwa agano la Kitabu kuwa wasiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila Haki tu? Nao wamekwisha soma yaliomo humo. Na nyumba ya Akhera ni bora kwa wanao jikinga na maasi. Basi je, hamtii akilini?
Surah Al-Araf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And there followed them successors who inherited the Scripture [while] taking the commodities of this lower life and saying, "It will be forgiven for us." And if an offer like it comes to them, they will [again] take it. Was not the covenant of the Scripture taken from them that they would not say about Allah except the truth, and they studied what was in it? And the home of the Hereafter is better for those who fear Allah, so will you not use reason?
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na wakafuatia baada yao kizazi kibaya walio rithi Kitabu. Wakashika anasa za haya maisha duni, na wakasema: Tutasamehewa! Na ikiwajia tena anasa kama hiyo wataishika pia. Je, hawakufanyiwa agano la Kitabu kuwa wasiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila Haki tu? Nao wamekwisha soma yaliomo humo. Na nyumba ya Akhera ni bora kwa wanao jikinga na maasi. Basi je, hamtii akilini?
Baada ya hao tulio kwisha wataja na tukawagawa sehemu mbili, walifuatia waovu wakairithi Taurati kutokana na walio watangulia. Lakini hao hawakufanya yalio amrishwa humo. Kwani wao walishika starehe ya dunia badala ya Neno la Haki. Wakijiambia nafsi zao: Mwenyezi Mungu atatusamehe kwa tunayo yatenda! Wakitaraji maghfira, na ilhali kuwa yakiwajia kama yale waliyo yashika watayashika vile vile. Basi wao wamekuwa wameshikilia kuendelea na madhambi pamoja na kutaka kwao msamaha. Tena basi Mwenyezi Mungu anawatahayarisha kwa vile kutaka maghfira na huku wanaendelea na yao, akasema: Sisi tulichukua kwao ahadi katika Taurati - nao wameyasoma yaliomo humo - kuwa waseme kweli; nao wakasema uwongo! Na hakika neema za nyumba ya Akhera za wanao jikinga na maasi ni bora kuliko starehe za duniani! Basi je, mtaendelea na uasi wenu, wala hayaingii akilini mwenu kuwa neema hizo ni bora kwenu? Na mnakhiari badala yake hizo starehe za dunia?
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Wala hatukuwapa Vitabu wavisome, wala hatukuwatumia Mwonyaji kabla yako wewe.
- Nao husema: Angeli penda Mwingi wa Rehema tusingeli waabudu sisi. Hawana ujuzi wowote wa hayo!
- Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shaahidi wa kila kitu.
- Wakasema: Hatutokukhiari wewe kuliko ishara waziwazi zilizo tujia, na kuliko yule aliye tuumba. Basi hukumu
- Kadhaalika; na tukawarithisha hayo Wana wa Israili.
- Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo elekezeni nyuso zenu
- Bali Yeye ndiye mtakaye mwomba, naye atakuondoleeni mnacho mwombea akipenda. Na mtasahau hao mnao wafanya
- Na kwa mji huu wenye amani!
- Basi wakigeuka, wewe sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Mimi namtegemea Yeye,
- Siku ambayo ardhi itatikiswa na milima pia, na milima itakuwa kama tifutifu la mchanga!
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Araf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Araf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Araf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers