Surah Hud aya 17 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّهِ وَيَتْلُوهُ شَاهِدٌ مِّنْهُ وَمِن قَبْلِهِ كِتَابُ مُوسَىٰ إِمَامًا وَرَحْمَةً ۚ أُولَٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۚ وَمَن يَكْفُرْ بِهِ مِنَ الْأَحْزَابِ فَالنَّارُ مَوْعِدُهُ ۚ فَلَا تَكُ فِي مِرْيَةٍ مِّنْهُ ۚ إِنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ﴾
[ هود: 17]
Basi je, mtu aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake Mlezi, inayo fuatwa na shahidi anaye toka kwake, na kabla yake kilikuwa Kitabu cha Musa kilicho kuwa mwongozi na rehema - hao wanamuamini, na anaye mkataa katika makundi, basi Moto ndio pahala pa miadi yao. Basi usiwe na shaka juu ya hayo. Hii ni Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi; lakini watu wengi hawaamini.
Surah Hud in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
So is one who [stands] upon a clear evidence from his Lord [like the aforementioned]? And a witness from Him follows it, and before it was the Scripture of Moses to lead and as mercy. Those [believers in the former revelations] believe in the Qur'an. But whoever disbelieves in it from the [various] factions - the Fire is his promised destination. So be not in doubt about it. Indeed, it is the truth from your Lord, but most of the people do not believe.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Basi je, mtu aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake Mlezi, inayo fuatwa na shahidi anaye toka kwake, na kabla yake kilikuwa Kitabu cha Musa kilicho kuwa mwongozi na rehema - hao wanamuamini, na anaye mkataa katika makundi, basi Moto ndio pahala pa miadi yao. Basi usiwe na shaka juu ya hayo. Hii ni Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi; lakini watu wengi hawaamini.
Je, anaye kuwa anakwenda katika maisha yake kwa uangalifu na uwongofu kutokana na Mola wake Mlezi, na anaitaka Haki kwa kuifanyia ikhlasi, pamoja naye anaye shahidi anaye mshuhudia kuwa kweli katoka kwa Mwenyezi Mungu, naye shahidi huyo ni Qurani, na shahidi wa kabla yake ni Kitabu cha Musa alicho kiteremsha Mwenyezi Mungu kiwe ni uwongozi wa kufuatwa kwa aliyo yaleta, na ni rehema kwa wenye kukifuata, je, huyo ni sawa sawa na anaye kwenda katika maisha yake katika giza na upofu, hashughulikii ila starehe za duniani tu na pumbao lake? Hao walio tajwa mwanzo ndio wale ambao Mwenyezi Mungu ameyatia nuru macho yao. Wanamuamini Nabii huyu, na Kitabu alicho teremshiwa. Na wenye kumkataa wakakusanyika na kujiunga dhidi yake, basi Moto ndio pahali pa miadi yao Siku ya Kiyama. Ewe Nabii! Usiwe na shaka na hii Qurani. Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Haingii upotovu. Lakini watu wengi wanapotezwa na matamanio, basi hawaamini kama iwapasavyo. Mwenyezi Mungu amemuamrisha Nabii s.a.w. asitie shaka, si kwa kuwa yawezekana kuwa yeye awe na shaka, lakini ni kuashiria kuwa walio kuwa duni yake Nabii wajilinde wasiache shaka ikaingia nyoyoni mwao.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na Musa akawateuwa watu sabiini katika kaumu yake kwa miadi yetu. Na ulipo fika mtetemeko
- Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye.
- Na alipo kwisha watengenezea mahitaji yao akakitia kikopo cha kunywea maji katika mzigo wa nduguye
- Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama maji tuliyo yateremsha kutoka mbinguni, kisha yakachanganyika
- Enyi mlio amini! Rukuuni na msujudu, na muabuduni Mola wenu Mlezi, na tendeni mema, ili
- Wala wewe hukuwa upande wa magharibi tulipo mpa Musa amri, wala hukuwa katika walio hudhuria.
- Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu,
- Na wewe fuata yanayo funuliwa kwako kwa wahyi. Na vumilia mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu, na
- Njia ya Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake Yeye tu viliomo mbinguni na katika ardhi. Jueni
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Hud with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Hud mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Hud Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers