Surah Furqan aya 2 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا﴾
[ الفرقان: 2]
Ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, wala hakuwa na mwana, wala hakuwa na mshirika katika ufalme, na akaumba kila kitu na akakikadiria kwa kipimo.
Surah Al-Furqan in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
He to whom belongs the dominion of the heavens and the earth and who has not taken a son and has not had a partner in dominion and has created each thing and determined it with [precise] determination.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, wala hakuwa na mwana, wala hakuwa na mshirika katika ufalme, na akaumba kila kitu na akakikadiria kwa kipimo.
Yeye Subhanahu ndiye peke yake aliye miliki mbingu na ardhi, aliye takasika na haja ya kuwa na mwana, wala hakuwa na mshirika wowote katika ufalme wake. Na Yeye kaumba kila kitu na akakipima kwa kipimo baraabara kwa sharia zake ili kiweze kutimiza waajibu wake kwa nidhamu. -Ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, wala hakuwa na mwana, wala hakuwa na mshirika katika ufalme, na akaumba kila kitu na akakikadiria kwa kipimo.- Ilimu ya sayansi ya sasa imethibitisha kuwa vitu vyote vinakwenda kwa mujibu wa hukumu za uumbaji wake, na maendeleo yake namna mbali mbali kwa kufuata mpango madhubuti ambao hapana mwenye uwezo juu yake ila Muumbaji mwenye uwezo Mwenye kuanzisha kila kitu. Kwani katika kuwa kwake imebainika kuwa vitu vyote viumbe vyote na vinga khitalifiana umbo lake na sura yake kwa hakika vinatokana na madda chache za asli za kuhisabika, na hisabu ya madda hizo (elements) zinakaribia mia, nazo ni 96 zinazo juulikana mpaka sasa. Nazo zina khitalifiana kwa sifa zao za maumbile (physically ) na za Al Kimyaa (Chemically), na pia katika uzito wake wa chembe (Atomic Weight). Zinaanza kwa madda asli (element) Nambari 1. Nayo ni Hydrogen yenye Atomic weight 1, na kuishia na element ya nambari 96, Borium, ambayo atomic weight yake bado haijuulikani. Na element ya mwisho katika sayansi ni Uranium na atomic weight yake ni 238.57. Na hizi elements hujengeka na kufanyika Compounds kwa mujibu wa kanuni madhubuti zisio weza kuepukwa. Hali kadhaalika mimea na wanyama. Kila mmoja wao amegawika katika koo na makundi na namna (orders, families, species and sub-species) zinazo geuka sifa zake kwa madaraja ya viumbe vilivyo hai mpaka kuishia viumbe vyenye Khalaya au Cell moja (unicellular) kama microbes mpaka viumbe vyenye cells nyingi (multi- cellular) mpaka kufikia binaadamu, naye ndiye aliye kamilika kuliko wote. Na kila namna ya hizi sifa maalumu zinarithika katika kundi kizazi baada ya kizazi. Na yote haya yanakwenda kufuata kanuni na mipango iliyo thibiti madhubuti inayo onyesha kwa uwazi utukufu wa Mwenye kuumba na uwezo wake. Ametakasika, Subhanahu na ametukuka na hao wanao mshirikisha naye.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Sema: Mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume. Na wakigeuka basi Mwenyezi Mungu hawapendi makafiri.
- Kwa hakika wanao rudi nyuma baada ya kwisha wabainikia uwongofu, Shetani huyo amewashawishi na amewaghuri.
- Huenda tutawafuata wachawi wakiwa wao ndio watakao shinda.
- Na tukawaokoa walio amini na wakawa wanamcha-mngu.
- Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama,
- Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?
- Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?
- Hukuwa wewe ila ni mwonyaji.
- Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye.
- (Akaambiwa): Ewe Ibrahim! Wachilia mbali haya! Kwa hakika amri ya Mola wako Mlezi imekwisha kuja,
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Furqan with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Furqan mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Furqan Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers