Surah Yunus aya 5 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿هُوَ الَّذِي جَعَلَ الشَّمْسَ ضِيَاءً وَالْقَمَرَ نُورًا وَقَدَّرَهُ مَنَازِلَ لِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَالْحِسَابَ ۚ مَا خَلَقَ اللَّهُ ذَٰلِكَ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ﴾
[ يونس: 5]
Yeye ndiye aliye lijaalia jua kuwa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hisabu. Mwenyezi Mungu hakuviumba hivyo ila kwa Haki. Anazipambanua Ishara kwa watu wanao jua.
Surah Yunus in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
It is He who made the sun a shining light and the moon a derived light and determined for it phases - that you may know the number of years and account [of time]. Allah has not created this except in truth. He details the signs for a people who know
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Yeye ndiye aliye lijaalia jua kuwa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hisabu. Mwenyezi Mungu hakuviumba hivyo ila kwa Haki. Anazipambanua Ishara kwa watu wanao jua.
Na Mola wenu Mlezi ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akalifanya jua litoe mwanga, na mwezi utoe nuru. Na akajaalia mwezi uwe na vituo ili vikusaidieni kuweza kupima nyakati zenu, na mjue idadi ya miaka na hisabu. Na wala Mwenyezi Mungu hakuumba hayo ila kwa hikima. Na Yeye Subhanahu katika Kitabu chake anazikunjua Ishara zenye kuonyesha Ungu wake na ukamilifu wa uwezo wake, ili mpate kuzingatia kwa akili zenu, na mkubali kwa yanayo hitajia ujuzi. Aya hii ya 5 inahakikisha ukweli wa kisayansi ambao haukujuulikana na hiyo sayansi ila hivi mwishoni. Hapo kwanza haukujuulikana, nao ni kuwa jua ni umbo lenye kuwaka moto, na ndio chanzo cha nguvu za kufanyia kazi zote, kwa Kiarabu huitwa taaqa, na kwa Kiingereza Energy, na kwa Kiswahili cha sasa Nishati. Katika nguvu hizo ni huo Mwangaza na Joto. Ama mwezi hauwaki moto, bali unarudisha mwangaza wa jua, kama kioo, kwa hivyo huonekana una nuru. Kwa hivyo Subhanahu ameeleza kuwa jua lina mwangaza wa asli, na mwezi unatoa nuru tu. Na Aya hii imeashiria hakika ya nyendo za falaki, nayo ni kuwa mwezi unaizunguka ardhi, na kila siku unakuwa katika mahala fulani kwa mintarafu ya dunia. Ukimaliza mzunguko wake ndio unatimia mwezi, huu wa siku 30 au 29. Kwa hivyo tunaweza kujua kiasi cha mwaka, na kwa hivyo twaweza kujua hisabu za miaka, miezi na siku.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na mwezi utapo patwa,
- Na kaumu ngapi tuliziangamiza zilizo kuwa na mapambo mazuri zaidi na wazuri zaidi kwa kuwatazama!
- Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa!
- Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na
- Na Sisi hakika tunajua kwamba wanasema: Yuko mtu anaye mfundisha. Lugha ya huyo wanaye muelekezea
- Na kifua changu kina dhiki, na ulimi wangu haukunjuki vyema. Basi mtumie ujumbe Harun.
- Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake walio deka kwa starehe walisema:
- Na wakaomba ushindi, na akashindwa kila jabari mkaidi,
- Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa wewe ni miongoni
- Na kwa hakika tulimpa Musa uwongofu, na tukawarithisha Wana wa Israili Kitabu,
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Yunus with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Yunus mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Yunus Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



