Surah Maidah aya 2 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُحِلُّوا شَعَائِرَ اللَّهِ وَلَا الشَّهْرَ الْحَرَامَ وَلَا الْهَدْيَ وَلَا الْقَلَائِدَ وَلَا آمِّينَ الْبَيْتَ الْحَرَامَ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّن رَّبِّهِمْ وَرِضْوَانًا ۚ وَإِذَا حَلَلْتُمْ فَاصْطَادُوا ۚ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ أَن صَدُّوكُمْ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ أَن تَعْتَدُوا ۘ وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۖ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ﴾
[ المائدة: 2]
Enyi mlio amini! Msivunje hishima ya alama ya Dini ya Mwenyezi Mungu wala mwezi mtakatifu, wala wanyama wanao pelekwa Makka kuchinjwa, wala vigwe vyao, wala wanao elekea kwendea Nyumba Takatifu, wakitafuta fadhila na radhi za Mola wao Mlezi. Na mkisha toka Hija yenu basi windeni. Wala kuwachukia watu kwa kuwa wali- kuzuilieni kufika Msikiti mtakatifu kusikupelekeeni kuwafanyia uadui. Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
Surah Al-Maidah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
O you who have believed, do not violate the rites of Allah or [the sanctity of] the sacred month or [neglect the marking of] the sacrificial animals and garlanding [them] or [violate the safety of] those coming to the Sacred House seeking bounty from their Lord and [His] approval. But when you come out of ihram, then [you may] hunt. And do not let the hatred of a people for having obstructed you from al-Masjid al-Haram lead you to transgress. And cooperate in righteousness and piety, but do not cooperate in sin and aggression. And fear Allah; indeed, Allah is severe in penalty.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Enyi mlio amini! Msivunje hishima ya alama ya Dini ya Mwenyezi Mungu wala mwezi mtakatifu, wala wanyama wanao pelekwa Makka kuchinjwa, wala vigwe vyao, wala wanao elekea kwendea Nyumba Takatifu, wakitafuta fadhila na radhi za Mola wao Mlezi. Na mkisha toka Hija yenu basi windeni. Wala kuwachukia watu kwa kuwa wali- kuzuilieni kufika Msikiti mtakatifu kusikupelekeeni kuwafanyia uadui. Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
Enyi Waumini! Msivunje hishima ya alama ya Dini ya Mwenyezi Mungu, yaani ibada alizo amrisha Mwenyezi Mungu, kama ibada za Hija wakati wa Ihram, na sharia na hukumu nyenginezo. Wala msivunje hishima ya miezi mitakatifu kwa kuzua vita katika miezi hiyo. Wala msipinge wanyama wanao pelekwa Makka, kwa kupokonya au kuzuia wasifike huko, wala msiwavue vigwe walivyo fungwa shingoni mwao kuwa ni alama kuwa wamekusudiwa kupelekwa Nyumba Takatifu, na kuwa watakuwa dhabihu wa Hija. Wala msiwapinge wanao kusudia kwenda Hija nao wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Na mkisha vua Ihram na mkatoka kwenye eneo la Alharam, basi mnaweza kuwinda mtakavyo. Wala msipelekewe na chuki yenu kubwa kwa wale walio kuzuieni kufika kwenye Msikiti wa Makka mkawafanyia uadui. Enyi Waumini! Saidianeni katika kutenda kheri na mambo yote ya utiifu, wala msisaidiane katika maasi, na kupindukia mipaka aliyo iweka Mwenyezi Mungu. Na ogopeni adhabu ya Mwenyezi Mungu na nguvu zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuwaadhibu wale wanao mkosa. Mwenye kuhiji akisha -harimiya- (yaani kunuia kuhiji) huwa haramu kwake baadhi ya mambo, kama kuvaa nguo iliyo shonwa, kukata nywele, kuwinda, n.k. mpaka amalize -Ihram- nako ndio kwisha ibada ya Hija.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Au mkasema: Lau kuwa tumeteremshiwa sisi Kitabu tungeli kuwa waongofu zaidi kuliko wao. Basi imekufikieni
- Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni. Na tufanyapo tena basi kweli sisi ni wenye kudhulumu.
- Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi.
- Basi ukawafikia uovu wa waliyo yatenda, na waliyo kuwa wakiyakejeli yakawazunguka.
- Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi.
- Sema: Kila mmoja anafanya kwa namna yake. Na Mola wenu Mlezi anajua aliye ongoka katika
- Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye kumbushwa kwa Ishara za Mola wake Mlezi,
- Basi naapa kwa Mola wako Mlezi! Kwa yakini tutawakusanya wao pamoja na mashet'ani; kisha tutawahudhurisha
- Badala ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Wametupotea, bali tangu zamani hatukuwa tukiomba kitu! Hivyo ndivyo Mwenyezi
- Nao huwazuia watu, na wao wenyewe wanajitenga nayo. Nao hawaangamizi ila nafsi zao tu, wala
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Maidah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Maidah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Maidah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers