Surah Maidah aya 3 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللَّهِ بِهِ وَالْمُنْخَنِقَةُ وَالْمَوْقُوذَةُ وَالْمُتَرَدِّيَةُ وَالنَّطِيحَةُ وَمَا أَكَلَ السَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيْتُمْ وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ وَأَن تَسْتَقْسِمُوا بِالْأَزْلَامِ ۚ ذَٰلِكُمْ فِسْقٌ ۗ الْيَوْمَ يَئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن دِينِكُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ ۚ الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيْرَ مُتَجَانِفٍ لِّإِثْمٍ ۙ فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ﴾
[ المائدة: 3]
Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aliye kufa kwa kunyongeka koo, na aliye kufa kwa kupigwa, na aliye kufa kwa kuanguka, na aliye kufa kwa kupigwa pembe, aliye liwa na mnyama, ila mkimdiriki kumchinja. Na pia ni haramu kula nyama aliye chinjiwa masanamu. Na ni haramu kupiga ramli. Hayo yote ni upotovu. Leo walio kufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu.
Surah Al-Maidah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Prohibited to you are dead animals, blood, the flesh of swine, and that which has been dedicated to other than Allah, and [those animals] killed by strangling or by a violent blow or by a head-long fall or by the goring of horns, and those from which a wild animal has eaten, except what you [are able to] slaughter [before its death], and those which are sacrificed on stone altars, and [prohibited is] that you seek decision through divining arrows. That is grave disobedience. This day those who disbelieve have despaired of [defeating] your religion; so fear them not, but fear Me. This day I have perfected for you your religion and completed My favor upon you and have approved for you Islam as religion. But whoever is forced by severe hunger with no inclination to sin - then indeed, Allah is Forgiving and Merciful.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye chinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aliye kufa kwa kunyongeka koo, na aliye kufa kwa kupigwa, na aliye kufa kwa kuanguka, na aliye kufa kwa kupigwa pembe, aliye liwa na mnyama, ila mkimdiriki kumchinja. Na pia ni haramu kula nyama aliye chinjiwa masanamu. Na ni haramu kupiga ramli. Hayo yote ni upotovu. Leo walio kufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu.
Enyi Waumini! Mwenyezi Mungu amekuharimisheni kula nyamafu, yaani aliye kufa bila ya kuchinjwa kisharia. Na damu inayo tiririka, na nyama ya nguruwe, na yule ambaye wakati wa kuchinjwa ametajiwa jina lisilo kuwa la Mwenyezi Mungu, na aliye kufa kwa kunyongwa, au aliye pigwa mpaka akafa, au aliye kufa kwa kuanguka, au kwa kupigwa pembe, au kwa kuliwa na mnyama mwingine. Ama yule mnaye mdiriki angali yu hai naye ni mnyama wa halali kuliwa, mkamchinja, basi huyo ni halali kwenu. Mwenyezi Mungu ameharimisha kula wanyama walio tolewa sadaka au mhanga kwa masanamu. Na pia ameharimisha kuagua yaliyo ghaibu kwa uganga wa kupiga ramli, na mfano wa hayo. Kula chochote katika vilivyo tajwa kuwa ni haramu ni dhambi kubwa, na ni kutoka kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu. Tangu sasa tamaa ya makafiri kuiviza Dini yenu imekwisha potea. Basi msiwaogope kuwa watakushindeni, bali ogopeni kutofuata amri zangu. Leo nimekukamilishieni hukumu za Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu kwa kukupeni nguvu na kukuimarisheni, na nimekukhitarieni UISLAMU uwe ndiyo Dini. Lakini mwenye kulazimika kwa njaa akala kidogo katika hivyo vilivyo harimishwa, akala ili asife, bila ya kukusudia uasi, basi Mwenyezi Mungu humsamehe mtu huyo kwa kulazimika kula cha haramu asije akafa. Mwenyezi Mungu ni Mwenye huruma na rehema kwa alivyo halalisha. Hafi mnyama wenyewe ila kwa maradhi, na hayo maradhi humdhuru mwanaadamu akila nyama yake, na huenda maradhi mengine yakawa ya kuambukiza. Katika damu vimo vijidudu vya maradhi. Ama katika nyama ya nguruwe mna vitu kadhaa wa kadhaa vya kumdhuru mtu. Na vilivyo chinjwa kwa jina la asiye kuwa Mwenyezi Mungu, na walio chinjiwa masanamu au mashetani, hayo ni mambo ya ibada potovu. Na vilivyo nyongeka, na vilivyo anguka, na kupigwa pembe ni sawa na mfu, au mzoga, kwa kuwa vimekufa kwa vifo vibaya, na khasa kwa kuwa damu yake haikutoka imevilia humo humo.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na hakika tulikwisha watuma Mitume kwa kaumu zao, na wakawajia kwa hoja zilizo wazi. Tukawaadhibu
- Kisha tunakivutia kwetu kidogo kidogo.
- Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea.
- Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- Na walio hama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha wakauwawa au wakafa, bila ya shaka
- Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona.
- Basi naapa kwa maanguko ya nyota,
- Hawakumuadhimisha Mwenyezi Mungu anavyo stahiki kuadhimishwa. Hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mwenye kushinda.
- Basi Musa akawanyweshea; kisha akarudi kivulini, na akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi ni mhitaji
- Na makhazina, na vyeo vya hishima,
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Maidah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Maidah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Maidah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers