Surah Baqarah aya 208 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ﴾
[ البقرة: 208]
Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za She'tani; hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
O you who have believed, enter into Islam completely [and perfectly] and do not follow the footsteps of Satan. Indeed, he is to you a clear enemy.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za Shetani; hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi.
Enyi mlio amini! Na iwe baina yenu nyote amani na salama,wala msichochee chuki za kijahiliya na mengineyo kuleta sababu za ugomvi na khitilafu. Wala msipite katika njia ya Shetani anaye kupelekeeni kugawanyika, kwani yeye ni adui wenu aliye dhaahiri. Maneno haya ya Qurani ni wito kwa Waumini wote iwe baina yao salama na amani, na yanafahamisha kuwa vita na khasama ni katika mwendo wa kumfuata Shetani. Waumini wote wanaitwa wawe katika hali ya salama na wengineo, na wao baina yao kwa wao, wasipigane na wengine wala wasipigane wenyewe kwa wenyewe. Na maneno haya ya Qurani yanaonyesha kuwa mahusiano baina ya dola ya Kiislamu na nyenginezo ni salama, na huo ni msingi wa mwanzo wa dini zote za mbinguni. Wakati ilipo kuwa kanuni ya porini ndiyo inayo hukumu baina ya madola na kuwekea mipaka ya mahusiano yao, mwenye nguvu kumla mnyonge, Uislamu ulikuja na huu msingi wa kuamrisha kuwa mahusiano yawe ya Usalama. Pindi vikitokea vita basi viwe kwa ajili ya ulinzi na kuupinga uvamizi. Yaani ni kumlazimisha yule mwenye kufanya uadui awe mwenye usalama. Vita vilivyo ruhusiwa na Uislamu ni kuthibitisha nguzo za amani, na kuhakikisha uadilifu. Vita hivi ni vita vya salama, kwa ajili ya uadilifu na amani.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Ambao husema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumeamini, basi tufutie madhambi yetu, na tuepushe na
- Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
- Bila ya shaka lilikuwapo kundi katika waja wangu likisema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini; basi tusamehe
- Je, huwaoni wale walio ambiwa: Izuieni mikono yenu, na mshike Sala na mtoe Zaka. Na
- Watakabiliana wao kwa wao kuulizana.
- Hatukukunjulia kifua chako?
- Qur'ani ya Kiarabu isiyo na upogo, ili wamche Mungu.
- Jueni kuwa vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika.
- Watadumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipo kuwa apendavyo Mola wako Mlezi. Hakika
- Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu!
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



