Surah Nisa aya 22 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَلَا تَنكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُم مِّنَ النِّسَاءِ إِلَّا مَا قَدْ سَلَفَ ۚ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَمَقْتًا وَسَاءَ سَبِيلًا﴾
[ النساء: 22]
Wala msiwaoe wake walio waoa baba zenu, ila yaliyo kwisha pita. Hakika huo ni uchafu na uchukizo na ni njia mbaya.
Surah An-Nisa in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And do not marry those [women] whom your fathers married, except what has already occurred. Indeed, it was an immorality and hateful [to Allah] and was evil as a way.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Wala msiwaoe wake walio waoa baba zenu, ila yaliyo kwisha pita. Hakika huo ni uchafu na uchukizo na ni njia mbaya.
Wala nyinyi, watoto, msiwaoe wanawake walio wahi kuolewa na baba zenu. Jambo hilo ni uchafu na linachusha, na linakirihiwa na Mwenyezi Mungu na watu. Na hiyo ni njia ovu kabisa. Lakini Mwenyezi Mungu anasamehe yaliyo kwisha tendeka katika zama za ujahili. Waarabu katika zama za ujahili walikuwa na ada zisio mpa heshima mwanamke, bali zikimdhulumu sana, na zikikata makhusiano mema katika ukoo. Ilikuwa mtu akifa baba yake na akawa na wake wasio kuwa mama yake mzazi, akilazimishwa kuwaoa, au akiwarithi wake za baba yake bila ya ndoa mpya. Na ilikuwa mtu akimwacha mke basi humpokonya kwa dhulma na uadui mahari yote aliyo mpa. Na walikuwapo walio kuwa wakimzuia huyo mtlaka asiolewe na mtu mwengine, kwa jeuri na inda. Ukaja Uislamu, ukamlinda mwanamke na dhulma hii iliyo wazi, ukakataza kurithiwa mke, na kumpokonya mahari yake hata chembe, ijapo kuwa ni mali mengi, na ukakataza kumzuia mtalaka asiolewe, au kumkera ili apate kutaka yeye mke talaka kwa kutoa mali. Na katika mtindo wao Waarabu wa jahiliya ilikuwa yafaa mtu kumwoa aliye kuwa mke wa baba yake na akafarikiana naye kwa talaka au mfano wake. Uislamu ukakataza hayo, na ukauwita mtindo huo ni uchafu, kwa sababu ni jambo baya analo lichukia Mwenyezi Mungu na kila mwenye akili sawa. Huo ndio uadilifu wa Mwenyezi Mungu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Nao husema: Wanyama hawa na mimea hii ni mwiko. Hawatokula ila wale tuwapendao - kwa
- Kwa Ishara wazi na Vitabu. Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao,
- Jueni kuwa vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika.
- Je! Hazikuwa Aya zangu mkisomewa, na nyinyi mkizikanusha?
- Ukininyooshea mkono wako kuniuwa, mimi sitakunyooshea mkono wangu kukuuwa. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola
- Asaa Mola wake Mlezi, akikupeni talaka, akampa wake wengine badala yenu nyinyi, walio bora kuliko
- Na katika usiku pia mtakase, na baada ya kusujudu.
- Hakika amefanikiwa aliye itakasa,
- Na siku itapo simama Saa wakosefu wataapa kwamba hawakukaa duniani ila saa moja tu. Hivyo
- Je! Nini wanangojea ila Saa iwajie kwa ghafla na wala wao hawatambui?
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nisa with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nisa mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nisa Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers