Surah Baqarah aya 258 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِي حَاجَّ إِبْرَاهِيمَ فِي رَبِّهِ أَنْ آتَاهُ اللَّهُ الْمُلْكَ إِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ رَبِّيَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا أُحْيِي وَأُمِيتُ ۖ قَالَ إِبْرَاهِيمُ فَإِنَّ اللَّهَ يَأْتِي بِالشَّمْسِ مِنَ الْمَشْرِقِ فَأْتِ بِهَا مِنَ الْمَغْرِبِ فَبُهِتَ الَّذِي كَفَرَ ۗ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ﴾
[ البقرة: 258]
Hukumwona yule aliye hojiana na Ibrahim juu ya Mola wake Mlezi kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? Ibrahim alipo sema: Mola wangu ni yule ambaye huhuisha na kufisha. Yeye akasema: Mimi pia nahuisha na kufisha. Ibrahim akasema: Mwenyezi Mungu hulichomozesha jua mashariki, basi wewe lichomozeshe magharibi. Akafedheheka yule aliye kufuru; na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Have you not considered the one who argued with Abraham about his Lord [merely] because Allah had given him kingship? When Abraham said, "My Lord is the one who gives life and causes death," he said, "I give life and cause death." Abraham said, "Indeed, Allah brings up the sun from the east, so bring it up from the west." So the disbeliever was overwhelmed [by astonishment], and Allah does not guide the wrongdoing people.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Hukumwona yule aliye hojiana na Ibrahim juu ya Mola wake Mlezi kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? Ibrahim alipo sema: Mola wangu ni yule ambaye huhuisha na kufisha. Yeye akasema: Mimi pia nahuisha na kufisha. Ibrahim akasema: Mwenyezi Mungu hulichomozesha jua mashariki, basi wewe lichomozeshe magharibi. Akafedheheka yule aliye kufuru; na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.
Humwoni yule aliye pofuka asizione dalili za Imani akajadiliana na Ibrahim, rafiki wa Mwenyezi Mungu, katika uungu wa Mola wake Mlezi na Umoja wake, na vipi alivyo danganyika na ufalme wake alio pewa na Mola wake Mlezi hata akatoka kwenye nuru ya maumbile akaingia katika kiza cha ukafiri? Alipo sema Ibrahim: Mwenyezi Mungu huhuisha na hufisha, kwa kuitia roho katika kiwiliwili na kuitoa, yule mfalme kafiri akasema: Nami nahuisha na ninafisha kwa kusamehe na kuuwa. Basi Ibrahim akamwambia ili kuyakata majadiliano: Mwenyezi Mungu analichomozesha jua mashariki, basi wewe lileta litoke magharibi kama wewe ni mungu kama unavyo dai. Akahizika, na majadiliano yakakatika kwa nguvu za hoja zilizo kashifu udhaifu wake na kughurika kwake. Na Mwenyezi Mungu hawawezeshi wakaidi na wenye inadi kufuata Haki.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hao ndio walio waambia ndugu zao na wao wenyewe wakakaa kitako: Lau wengeli tut'ii wasingeli
- Na katika Ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Basi msilisujudie jua
- Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe.
- Na ikiwa ni makubwa kwako huku kukataa kwao, basi kama unaweza kutafuta njia ya chini
- Akasema: Niliona wasiyo yaona wao, nikashika gao katika unyao wa Mtume. Kisha nikalitupa. Na hivi
- Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa.
- Na Mola wako Mlezi anayajua yaliyo ficha vifua vyao, na wanayo yatangaza.
- Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyo barikiwa, na kwa hayo tukaotesha mabustani na nafaka za
- Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu,
- Akasema: Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia yako Iliyo Nyooka.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers