Surah Fatir aya 27 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ ثَمَرَاتٍ مُّخْتَلِفًا أَلْوَانُهَا ۚ وَمِنَ الْجِبَالِ جُدَدٌ بِيضٌ وَحُمْرٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهَا وَغَرَابِيبُ سُودٌ﴾
[ فاطر: 27]
Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na myeusi sana.
Surah Fatir in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Do you not see that Allah sends down rain from the sky, and We produce thereby fruits of varying colors? And in the mountains are tracts, white and red of varying shades and [some] extremely black.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na myeusi sana.
Ewe mwenye akili! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu anayateremsha maji kutoka mbinguni, na kwa maji hayo anatoa mazao yanayo khitalifiana rangi zake? Mengine ni mekundu na manjano, na matamu na machungu, mazuri na mabaya. Na katika milima, ipo milima yenye njia na mistari myeupe na myekundu, yenye kukhitalifiana pia kwa kukoza na kufifia. Ya kustaajabisha kitaalamu katika Aya hii tukufu sio tu kwa kukhitalifiana rangi mbali mbali katika milima, ambazo zinatokana na hizo sehemu za maadini zilizo fanya majabali, kama vile chuma huonyesha rangi yake nyekundu, na manganese na makaa ya mawe huonekana kwa rangi nyeusi, au shaba ambayo hudhihirisha rangi ya kijani n.k. Lakini ya kustaajabisha khasa ni kuunganisha baina ya kutoa matunda ya namna mbali mbali na hali miti yake inanyweshwa maji yale yale, na kuumbwa milima myekundu, na myeupe, na myeusi, na yote yana asli moja kwa kuundwa kwake. Wataalamu wa ilimu za tabaka za ardhi, Jiolojia, wanaita Magma. Na hii Magma moja inapo chomoza pahala mbali mbali katika ardhi, na penye vina mbali mbali (kwenda chini) katika ardhi kutoka juu basi hupatikana khitilafu katika muundo wake na hukusanyika kwa kurindika kuwa ni milima yenye maadini ya rangi mbali mbali. Na huu basi mwendo wa Mwenyezi Mungu ni mmoja. Kwani hakika asli ni moja, na matawi ndiyo yanakhitalifiana kwa kuonekana. Na katika haya yanapatikana manufaa na faida kwa binaadamu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na wakikukanusha basi walikanushwa Mitume wengine kabla yako walio kuja na hoja waziwazi na Vitabu
- Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Hivyo mnatuchukia kwa kuwa tumemuamini Mwenyezi Mungu na tuliyo teremshiwa
- Na walio kufuru wanasema: Wewe hukutumwa. Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na
- Kila nafsi itaonja mauti. Kisha mtarudishwa kwetu.
- Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu
- Basi ingieni milango ya Jahannamu, humo mdumu. Ni maovu mno makaazi ya wafanyao kiburi!
- Ukikupata wema unawachukiza, na ukikusibu msiba, wao husema: Sisi tuliangalia mambo yetu vizuri tangu kwanza.
- Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi.
- Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia. Na mema yanayo bakia ni bora
- Na wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu baada ya hayo, basi hao ndio madhaalimu.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Fatir with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Fatir mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Fatir Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers