Surah Al Imran aya 28 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿لَّا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللَّهِ فِي شَيْءٍ إِلَّا أَن تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً ۗ وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّهُ نَفْسَهُ ۗ وَإِلَى اللَّهِ الْمَصِيرُ﴾
[ آل عمران: 28]
Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na anaye fanya hivyo, basi hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ila ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni naye. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.
Surah Al Imran in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Let not believers take disbelievers as allies rather than believers. And whoever [of you] does that has nothing with Allah, except when taking precaution against them in prudence. And Allah warns you of Himself, and to Allah is the [final] destination.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na anaye fanya hivyo, basi hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ila ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao. Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni naye. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.
Ikiwa basi ni Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala ndiye Yeye peke yake Mmiliki wa mamlaka, anatukuza na kuangusha, na katika mikono yake pekee ipo kheri, na uumbaji, na riziki, basi haifai kwa Waumini kuwafanya wasio kuwa Waumini wawe na utawala juu yao, wakauwacha msaada wa Waumini wenzao. Kwani wakifanya haya inakuwa wanaivunja Dini, na wanawaletea maudhi wenye Dini, na ni kuudhoofisha utawala na udugu wa Kiislamu. Na mwenye kufuata njia hii basi kwa Mwenyezi Mungu Mmiliki wa mamlaka yote hana lake jambo. Wala haimfalii Muumini kuridhia kuwapa utawala na ulinzi makafiri ila awe hana hila. Hapo basi anaweza kujikinga na madhara yao kwa kuonyesha utiifu kwao. Ni juu ya Waumini wawe daima katika ulinzi wa Kiislamu, kwani huo ndio ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Na watahadhari wasitoke kwenye ulinzi wa Mwenyezi Mungu kuuendea ulinzi mwenginewe asije akawaadhibu kwa kuwaletea madhila baada ya utukufu. Na kwake Yeye ndio marejeo, wala hapana pa kukimbilia kutokana na madaraka yake duniani wala Akhera.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na wanapo kuona hawakuchukulii ila ni mzaha tu, na (wanasema): Ati ndiye huyu Mwenyezi Mungu
- Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu
- Na (waonye) siku tutakapo wainua mashahidi katika kila umma wakiwashuhudia kwa yanayo tokana na wao,
- Wakasema: Tunaabudu masanamu, daima tunayanyenyekea.
- Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni.
- Mola Mlezi wao, akayakubali maombi yao akajibu: Hakika sipotezi kazi ya mfanya kazi miongoni mwenu,
- Nendeni mtoke, mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali yenu na nafsi zenu
- Na mkilipiza basi lipizeni sawa na vile mlivyo adhibiwa. Na ikiwa mtasubiri, basi hakika hivyo
- Na kwa usiku unapo pungua,
- Anajua viliomo katika mbingu na ardhi, na anajua mnayo yaficha na mnayo yatangaza. Na Mwenyezi
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Al Imran with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Al Imran mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Al Imran Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



