Surah Tawbah aya 29 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿قَاتِلُوا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حَتَّىٰ يُعْطُوا الْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ﴾
[ التوبة: 29]
Piganeni na wasio muamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharimishi alivyo harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa walio pewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa khiari yao, hali wamet'ii.
Surah At-Tawbah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Fight those who do not believe in Allah or in the Last Day and who do not consider unlawful what Allah and His Messenger have made unlawful and who do not adopt the religion of truth from those who were given the Scripture - [fight] until they give the jizyah willingly while they are humbled.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Piganeni na wasio muamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharimishi alivyo harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa walio pewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa khiari yao, hali wametii.
Enyi mlio amini! Wapigeni vita makafiri katika Watu wa Kitabu wasio muamini Mwenyezi Mungu kwa Imani iliyo sawa, wala hawakiri kuwa kuna kufufuliwa na kulipwa, wala hawayashiki aliyo yakataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawaishiki Dini ya Haki, nayo ni Uislamu. Wapigeni vita mpaka waamini, au watoe Jizya, nao wamenyenyekea na watiifu, si wenye kuasi, wasaidie katika kujenga mfuko wa Kiislamu. -Jizya- ni katika kipato muhimu katika madukhuli ya serikali ya Kiislamu. Kodi hii ilikuwa baina ya Dirham 8 na 40. Kila mtu mmoja katika Mayahudi na Wakristo na walio kuwa kama wao akitozwa Dirham 12. Akilazimishwa kulipa mwanamume aliye kwisha baalighi, na mzima wa mwili na akili, na kwa sharti awe na mali ya kuweza kutoa. Wanawake na watoto walisamehewa, na vile vile vizee. Kwa sababu hao hawapigwi vita. Wala hawatozwi vipofu na wasio jiweza, ila wakiwa matajiri. Kadhaalika hawatozwi mafakiri na masikini na watumwa. Wala hawakutakiwa kutoa mamonaki, yaani mapadri wanao jitenga na watu. Na asli ya kutozwa Jizya ni ulinzi wa wasio kuwa Waislamu. Kwa sababu Ahli Lkitaab, Watu wa Biblia, na walio kama wao, hawakulazimishwa kuingia vitani kulinda nchi wala kujilinda nafsi zao. Kwa hivyo ilikuwa ni haki wao watoe kodi kuwa ni badala ya ulinzi na manufaa mengine ya dola wanayo yapata na wanastarehea nayo. Pia ni badala ya wanacho kitoa Waislamu. Kwani Muislamu anatozwa ile khumsi (moja katika tano) ya ngawira, anatozwa Zaka ya mali, na Zaka ya Fitri, na kafara mbali mbali kwa kulipia makosa. Kwa hivyo ikawa hapana budi kuchukuliwa kodi kutokana kwa asiye kuwa Muislamu badala ya yote anayo yatoa Muislamu kwa maslaha ya wote na kwa ajili ya mafakiri wa wasio kuwa Waislamu. Wala haikukusudiwa kutozwa kodi kuwatia unyonge au kuwatia adabu. Kwani hayo hayaambatani na uadilifu wa Uislamu, wala hayakubaliani na makusudio yake mazuri.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Akijiona katajirika.
- (Firauni) akasema: Basi Mola wenu Mlezi ni nani, ewe Musa?
- Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume. Je, akifa au
- Ila wale walio subiri wakatenda mema. Hao watapata msamaha na ujira mkubwa.
- Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini?
- Yatima aliye jamaa,
- Na pia kina A'di na Thamud. Nanyi yamekwisha kubainikieni kutokana na maskani zao. Na Shet'ani
- Sema: Mimi nakuonyeni kwa Wahyi. Na viziwi hawasikii wito wanapo onywa.
- Basi yule bwana alipoona kanzu yake imechanwa kwa nyuma, alisema: Hakika haya ni katika vitimbi
- Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Tawbah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Tawbah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Tawbah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers