Surah Anbiya aya 44 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿بَلْ مَتَّعْنَا هَٰؤُلَاءِ وَآبَاءَهُمْ حَتَّىٰ طَالَ عَلَيْهِمُ الْعُمُرُ ۗ أَفَلَا يَرَوْنَ أَنَّا نَأْتِي الْأَرْضَ نَنقُصُهَا مِنْ أَطْرَافِهَا ۚ أَفَهُمُ الْغَالِبُونَ﴾
[ الأنبياء: 44]
Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka umri ukawa mrefu kwao. Je, hawaoni ya kwamba Sisi tunaifikia ardhi tukiipunguza ncha zake? Basi je! Hao ni wenye kushinda?
Surah Al-Anbiya in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
But, [on the contrary], We have provided good things for these [disbelievers] and their fathers until life was prolonged for them. Then do they not see that We set upon the land, reducing it from its borders? So it is they who will overcome?
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka umri ukawa mrefu kwao. Je, hawaoni ya kwamba Sisi tunaifikia ardhi tukiipunguza ncha zake? Basi je! Hao ni wenye kushinda?
Sisi hatufanyi haraka kuwaadhibu hawa kwa ukafiri wao, lakini tunawapururia na kuwastarehesha katika uhai wa dunia, kama tulivyo wastarehesha baba zao kabla yao, mpaka umri ukawa mrefu kwao. Je! Wanajitia upofu hawaoni yanao wazunguka wakaona kuwa Sisi tunaiendea nchi na tukaipunguza ncha zake kwa ushindi wa Waumini? Ni wao ndio wenye kushinda au Waumini ambao Mwenyezi Mungu amewaahidi kuwasaidia na kuwaunga mkono? Maoni ya wataalamu juu ya Aya 44: -Je, hawaoni ya kwamba Sisi tunaifikia ardhi tukiipunguza mipaka yake? Basi je! Hao ni wenye kushinda?-: Aya hii ni katika Aya za miujiza ya kisayansi katika Qurani Tukufu. Hii inaonyesha kuwa dunia si mduwara kaamili. Na wataalamu wa sayansi hawakutamakani kupima masafa ya dunia baraabara mpaka kiasi ya miaka 250 tu takriban, walipo ingia kikundi cha mabingwa walio khusika na ilimu ya kupima marefu baina ya daraja mbili za urefu longitudes. Na hayo kwa pahala mbali mbali duniani. Katika kupima huku ikadhihiri kuwa nusu ya kati ya dunia kwenye equator inazidi kuliko nusu ya poles kwa takriban kilomita 21.5. Yaani dunia imepungua katika ncha zake, yaani katika poles. Na inajuulikana maalumu kuwa sura ya dunia na masafa yake ndio msingi katika kuchorwa kwa ramani.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu!
- Sema: Mwaonaje ikikujieni adhabu ya Mwenyezi Mungu, au ikakufikieni hiyo Saa - mtamwomba asiye kuwa
- Na tukakuondolea mzigo wako,
- Akasema: Hakika mimi nachelea wasinikanushe.
- Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa!
- Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie.
- Nao watasema: Alhamdulillah, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye tutimizia ahadi yake, na
- (Tukamwambia:) Tengeneza nguo za chuma pana, na kadiria sawa katika kuunganisha. Na tendeni mema. Hakika
- Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim
- Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anbiya with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anbiya mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anbiya Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers