Surah Furqan aya 61 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿تَبَارَكَ الَّذِي جَعَلَ فِي السَّمَاءِ بُرُوجًا وَجَعَلَ فِيهَا سِرَاجًا وَقَمَرًا مُّنِيرًا﴾
[ الفرقان: 61]
Ametukuka aliye zijaalia nyota mbinguni, na akajaalia humo taa na mwezi unao ng'ara.
Surah Al-Furqan in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Blessed is He who has placed in the sky great stars and placed therein a [burning] lamp and luminous moon.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Ametukuka aliye zijaalia nyota mbinguni, na akajaalia humo taa na mwezi unao ngara.
Ametukuka Arrahman, Mwingi wa Rehema, na zimezidi fadhila zake. Ameziumba sayari mbinguni na akazijaalia na vituo vyake vya kupitia, na katika hizo akaumba jua kuwa ni taa yenye mwangaza, na mwezi wenye nuru. -Ametukuka aliye zijaalia nyota mbinguni, na akajaalia humo taa na mwezi unao ngara.- Aya hii tukufu inaashiria maana za ki-ilimu za sayansi zenye kukusanywa katika mpango wa ulimwengu alio uumba Mwenyezi Mungu, Aliye takasika, Aliye tukuka, na zikazidi fadhila zake. Na sisi tunashuhudia nyota za mbinguni kwa sura ya makundi ambayo takriban hayageuki sura na yangapitiliwa na karne, na Buruuj nayo ndio hayo makundi ya nyota, ni yale yale yanayo pitiwa mbele yake na jua katika mzunguko wake unavyo dhihiri kuizunguka ardhi. Hizo Buruuj ni kama vituo vya jua katika mzunguko wake katika mwaka. Na kila tatu katika hizo huwa ni musimu katika misimu ya mwaka. Nazo kwa kuzitaja moja moja kuanzia msimu wa Rabii (Spring) unao kuja baina ya siku za baridi na joto, ni kama ifuatavyo kwa majina ya Kiarabu na Kizungu: AlHaml (Aries, or Ram), Ath-thawr (Taurus), Aljawzaa (Gemini), Assarataan (Cancer), Al Asad (Leo), Assunbulah (Spica), Al Miizaan (Libra), Al-aqrab (Scorpion), Al Jadyu (Capricorn), Addalwu (Aquarius), AlHuut (Pisces). Na jua ni moja katika nyota zenye nguvu za kati na kati. Nalo kama nyota zilizo baki lina mwangaza wake mwenyewe wa dhati kwa vituko vya kichembechembe (atomic reaction) vinavyo tokea ndani yake. Basi miale ya jua inayo toka kwenye nguvu hizo huangukia juu ya sayari, na ardhi, na miezi, na vyombo vilio baki vya mbinguni ambavyo havina mwanga wa nafsi yao. Kwa hivyo navyo hutoa nuru. Basi jua ndio Taa inayo waka kwa nafsi yake. Ama mwezi unarudisha nuru ya mwanga wa jua kutokana na uso wake, kama kiyoo. Hakika kwa kusifiwa Jua kuwa ni Taa, na ukasifiwa mwezi kuwa unatoa nuru, ni ishara ya kuwa Jua ndio chanzo cha nguvu, nishati, (taaqah, Energy) za joto.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hakika tuliidhalilisha milima pamoja naye ikisabihi jioni na asubuhi pamoja naye.
- Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma.
- Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua.
- Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu
- Sema: Mnawaona hawa miungu wenu wa kishirikina mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu! Nionyesheni wameumba
- Hii ni ada ya Mwenyezi Mungu iliyo kuwa kwa wale walio pita zamani. Wala hutapata
- Jinsi Mola wangu Mlezi alivyo nisamehe, na akanifanya miongoni mwa walio hishimiwa.
- Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea.
- Na inapo teremshwa Sura wapo miongoni mwao wasemao: Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia
- Namna hivi ndivyo walivyo geuzwa walio kuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Furqan with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Furqan mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Furqan Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



