Surah Yunus aya 6 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿إِنَّ فِي اخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا خَلَقَ اللَّهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَّقُونَ﴾
[ يونس: 6]
Hakika katika kukhitalifiana usiku na mchana, na katika alivyo umba Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi, zipo Ishara kwa watu wanao mcha-Mngu.
Surah Yunus in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Indeed, in the alternation of the night and the day and [in] what Allah has created in the heavens and the earth are signs for a people who fear Allah
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Hakika katika kukhitalifiana usiku na mchana, na katika alivyo umba Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi, zipo Ishara kwa watu wanao mcha-Mngu.
Hakika katika kufuatana usiku na mchana na kukhitalifiana kwao, kwa kuzidi na kupungua, na katika uumbaji wa mbingu na ardhi na vitu vyote viliomo humo, zipo dalili zilizo wazi na hoja zilizo dhaahiri zenye kuhakikisha Ungu wa Mwenye kuumba, na uwezo wake. Hayo ni kwa wenye kutaka kuiepuka ghadhabu yake na wakaiogopa adhabu yake. Aya hii ya 6 inaashiria hakika inayo onekana, nayo kukhitalifiana urefu wa usiku na mchana kwa mwaka mzima katika pahala popote duniani. Na kadhaalika kufuatana mchana na usiku, na kuwa mchana ni wa kuangaza na kuonana, na usiku ni giza. Na maana ya hayo ni kuwa msingi wake ni kuwa dunia inazunguka wenyewe kwa wenyewe kama pia juu ya msumari wake, na vile vile inalizunguka jua. Na yote hayo ni dalili ya uwezo wa Mwenye kuumba katika kuanzisha uumbaji. Ujuzi wa mambo hayo wakati wa Mtume s.a.w. haukuwepo. Na hii ni dalili nyengine ya kwamba haya hayakuwa ila ni wahyi, ufunuo, ulio toka kwa Mwenyezi Mungu kumpa Mtume s.a.w.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana na kukaririwa; husisimua kwacho ngozi za
- Na walisema: Kwa nini hakutuletea muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi? Je! Haikuwafikilia dalili wazi
- Na anaye subiri, na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.
- Mabustani na mizabibu,
- Na wakaja watu wa mji ule nao furahani.
- Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na ardhi. Na
- Na wanao mwitikia Mola wao Mlezi, na wakashika Sala, na mambo yao yakawa ni kwa
- Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli,
- Sema: Tembeeni ulimwenguni, kisha mtazame ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha.
- Walisema: Je! Tukisha kufa tukawa udongo na mifupa ndio tutafufuliwa?
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Yunus with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Yunus mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Yunus Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers