Surah Yusuf aya 76 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿فَبَدَأَ بِأَوْعِيَتِهِمْ قَبْلَ وِعَاءِ أَخِيهِ ثُمَّ اسْتَخْرَجَهَا مِن وِعَاءِ أَخِيهِ ۚ كَذَٰلِكَ كِدْنَا لِيُوسُفَ ۖ مَا كَانَ لِيَأْخُذَ أَخَاهُ فِي دِينِ الْمَلِكِ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّهُ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ وَفَوْقَ كُلِّ ذِي عِلْمٍ عَلِيمٌ﴾
[ يوسف: 76]
Basi akaanza kwenye mizigo yao kabla ya mzigo wa nduguye. Kisha akakitoa katika mzigo wa nduguye. Hivi ndivyo tulivyo mpangia Yusuf. Hakuweza kumzuia nduguye kwa sharia ya mfalme isipo kuwa alivyo taka Mwenyezi Mungu. Tunawatukuza kwenye vyeo tuwatakao; na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi.
Surah Yusuf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
So he began [the search] with their bags before the bag of his brother; then he extracted it from the bag of his brother. Thus did We plan for Joseph. He could not have taken his brother within the religion of the king except that Allah willed. We raise in degrees whom We will, but over every possessor of knowledge is one [more] knowing.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Basi akaanza kwenye mizigo yao kabla ya mzigo wa nduguye. Kisha akakitoa katika mzigo wa nduguye. Hivi ndivyo tulivyo mpangia Yusuf. Hakuweza kumzuia nduguye kwa sharia ya mfalme isipo kuwa alivyo taka Mwenyezi Mungu. Tunawatukuza kwenye vyeo tuwatakao; na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi.
Shauri ikaishia ipekuliwe mizigo, na ikawa lazima kufanya mambo baraabara ili isionekane kuwa kuna mpango ulio pangwa. Yusuf mwenyewe ndiye aliye fanya uchunguzi, baada ya kwisha tengeza mambo. Akaanza kupekua mizigo ya wale ndugu kumi, kisha ndio akaingia kuupekua mzigo wa nduguye. Humo akakitoa kile kikopo, na kwa hivyo hila yake ikafuzu. Akawa na haki kwa hukumu ya nduguze kumshika Bin-yamini. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyo mpangia mambo Yusuf. Hakuwa anaweza yeye kumshika nduguye kwa mujibu wa sharia ya mfalme wa Misri tu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Naye alitaka. Basi tulimpangia mambo Yusuf, na tukamwezesha kuzirekibisha sababu na mipango baraabara na hila nzuri. Na haya ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu, ambaye humtukuza katika vyeo vya ujuzi amtakaye. Na juu ya kila mwenye ilimu yupo mwenye kumzidia katika ujuzi!
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni.
- Basi tukawatoa katika mabustani na chemchem,
- Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,
- Wanao toa mali zao kwa Njia ya Mwenyezi Mungu, kisha hawafuatishii masimbulizi wala udhia kwa
- Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa,
- Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho.
- Msifanye wito wa Mtume baina yenu kama wito wa nyinyi kwa nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu
- Na pale Shet'ani alipo wapambia vitendo vyao, na akawaambia: Hapana watu wa kukushindeni hii leo,
- Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo vifanya!
- Hao ndio walio na uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio wenye kufanikiwa.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Yusuf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Yusuf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Yusuf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers