Surah Maidah aya 8 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ لِلَّهِ شُهَدَاءَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَىٰ أَلَّا تَعْدِلُوا ۚ اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۖ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۚ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴾
[ المائدة: 8]
Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.
Surah Al-Maidah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
O you who have believed, be persistently standing firm for Allah, witnesses in justice, and do not let the hatred of a people prevent you from being just. Be just; that is nearer to righteousness. And fear Allah; indeed, Allah is Acquainted with what you do.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.
Enyi Waumini! Jitahidini kutimiza haki za Mwenyezi Mungu, na shuhudieni kwa haki baina ya watu. Chuki zenu kubwa kwa watu fulani zisikupelekeeni mkaacha kuwafanyia uadilifu. Bali jilazimisheni uadilifu, kwani hiyo ndiyo njia ya kupelekea kumcha Mwenyezi Mungu, na kuepukana na ghadhabu yake. Na mcheni Mwenyezi Mungu katika mambo yenu yote; kwani Yeye, Sub hanahu, anayajua vilivyo yote mnayo yafanya, naye atakulipeni kwayo. Uislamu unalingania uadilifu moja kwa moja, sawa kwa rafiki na adui.Haifai chuki ikakupelekea kudhulumu. Na hayo unapo amiliana na watu, na kuamiliana baina ya dola ya Kiislamu na dola nyenginezo. Na kumfanyia uadilifu adui kunaambiwa na Qurani kuwa ni karibu zaidi na uchamngu na usafi wa kidini. Lau kuwa wasia huu ungeli tumiwa katika sharia za baina ya madola basi pasingeli kuwapo vita. Kama kila dini ina kitambulisho chake na alama, basi kitambulisho cha Uislamu ni Dini ya Mungu Mmoja na Uadilifu.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Naapa kwa Zama!
- Hichi kitabu chetu kinasema juu yenu kwa haki. Hakika Sisi tulikuwa tukiyaandika mliyo kuwa mkiyatenda.
- Basi inakuwaje unapo wasibu msiba kwa sababu ya yale iliyo tanguliza mikono yao? Hapo tena
- Wanakuapieni Mwenyezi Mungu ili kukuridhisheni nyinyi, hali ya kuwa wanao stahiki zaidi kuridhishwa ni Mwenyezi
- Na tungeli penda tungeli yafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wange ionaje?
- Na enyi watu wangu! Kukhalifiana nami kusikupelekeeni hata mkasibiwa kama walivyo sibiwa watu wa Nuhu,
- Wakasema wale wanao jivuna: Sisi tunayakataa hayo mnayo yaamini.
- Sema: Enyi waja wangu mlio amini! Mcheni Mola wenu Mlezi. Wale wafanyao wema katika dunia
- Asaa Mola wake Mlezi, akikupeni talaka, akampa wake wengine badala yenu nyinyi, walio bora kuliko
- Je, huwaoni wale walio ambiwa: Izuieni mikono yenu, na mshike Sala na mtoe Zaka. Na
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Maidah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Maidah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Maidah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



