Surah Yasin aya 80 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿الَّذِي جَعَلَ لَكُم مِّنَ الشَّجَرِ الْأَخْضَرِ نَارًا فَإِذَا أَنتُم مِّنْهُ تُوقِدُونَ﴾
[ يس: 80]
Aliye kujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha.
Surah Ya-Sin in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
[It is] He who made for you from the green tree, fire, and then from it you ignite.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Aliye kujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha.
Aliye kuumbieni moto kutoka mti mbichi, baada ya kwisha kauka. Nguvu za jua zinaingia ndani ya mimea kwa wasita wa mwangaza. Khalaya zenye madda ya kijani katika mimea Chlorophyl ndizo zinafyonza Carbon dioxide kutokana na hewa, na hii huchanganyika na maji yanayo fonzwa na mimea, na kufanyika Carbohydrates kwa kuathiriwa na nguvu zinazo tokana na mwangaza wa jua. Tena hufanyika mbao, kuni, ambazo sehemu kubwa ni muundo wa kimyaa wa Carbon na Hydrogen na Oxygen. Na kutokana na kuni hizi hufanyika makaa haya ya miti tuyatumiayo. Ukiyachoma makaa hutoka nguvu zilizo kuwamo ndani yake kwa ajili ya kupikia, na kwa kazi nyingi nyenginezo. Na makaa ya mawe si chochote ila ni hiyo hiyo mimea na miti iliyo kuwa na kufanyika kama ilivyo elezwa, na kisha ikazikika kwa njia fulani na kugeuka baada ya kupita mamilioni ya miaka kuwa makaa ya mawe, kwa kuathirika na hali za geology kama joto au mdidimizo au menginewe. Na yapasa kuzingatia kuwa kutajwa katika Aya hii -mti wa kijani- si bure, bali ni ishara ya hiyo Chlorophyll ya kijani ambayo ni lazima kwa ajili ya kuimeza Carbon dioxide katika mimea.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala kufikia urefu wa
- Na wanapo kuona hawakuchukulii ila ni mzaha tu, na (wanasema): Ati ndiye huyu Mwenyezi Mungu
- Basi alipo ufikia aliitwa kutoka ng'ambo ya bonde la kuliani katika eneo lilio barikiwa kutoka
- Na walio mcha Mola wao Mlezi wataongozwa kuendea Peponi kwa makundi, mpaka watakapo fikilia, nayo
- Na wao wana kisasi juu yangu, kwa hivyo naogopa wasije kuniuwa.
- Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na
- Na Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa
- Ala! Sasa? Na hali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa mafisadi!
- Na kitupe kilicho katika mkono wako wa kulia; kitavimeza walivyo viunda. Hakika walivyo unda ni
- Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Yasin with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Yasin mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Yasin Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



