Surah Baqarah aya 89 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَلَمَّا جَاءَهُمْ كِتَابٌ مِّنْ عِندِ اللَّهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ وَكَانُوا مِن قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَمَّا جَاءَهُم مَّا عَرَفُوا كَفَرُوا بِهِ ۚ فَلَعْنَةُ اللَّهِ عَلَى الْكَافِرِينَ﴾
[ البقرة: 89]
Na kilipo wajia Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha waliyo nayo - na wao walikuwa wakitafutia ushindi kuwashinda makafiri - yalipo wajia yale waliyo kuwa wakiyajua waliyakanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu juu ya wakanushao!
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And when there came to them a Book from Allah confirming that which was with them - although before they used to pray for victory against those who disbelieved - but [then] when there came to them that which they recognized, they disbelieved in it; so the curse of Allah will be upon the disbelievers.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na kilipo wajia Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha waliyo nayo - na wao walikuwa wakitafutia ushindi kuwashinda makafiri - yalipo wajia yale waliyo kuwa wakiyajua waliyakanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu juu ya wakanushao!
Na Mtume wetu alipo wajia na Qurani, nayo ni Kitabu kilicho toka kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha Taurati walio teremshiwa wao, na wakajua kutokana na hiyo Taurati ukweli uliomo katika Kitabu hichi (Qurani) walikataa kwa inadi na uhasidi tu, kwa sababu yamekuja hayo kutokana na Mtume asiye kuwa wa taifa lao la Wana wa Israili, juu ya kuwa kabla yake walipo kuwa wakipambana na makafiri washirikina ikiwa mpambano wa vita au majadiliano, wakitaja kuwa Mwenyezi Mungu atakuja wanusuru wao kwa kumtuma Nabii wa mwisho aliye bashiriwa katika Kitabu chao, na ambaye sifa zake zimewafikiana kabisa moja kwa moja na sifa za Muhammad. Jueni basi laana ya Mwenyezi Mungu iko juu ya watu wa namna hii wenye inda na ukanushi. (Mwenyezi Mungu alimwambia Musa: -Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe...mtu asiye sikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake.- --Kumbukumbu la Torati 18.18-22. Maana ya haya ni: Taurati inasema kwamba Nabii Musa aliambiwa na Mungu kwamba atawaletea Nabii kutokana na ndugu za Wana wa Israili, yaani Waarabu. Na asiye mfuata Nabii huyo Mwenyezi Mungu atamuadhibu.)
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Enyi mlio pewa Kitabu! Aminini tuliyo yateremsha yenye kusadikisha yale mliyo nayo, kabla hatujazigeuza nyuso
- Au wamepata miungu katika ardhi inayo fufua?
- Sisi tumewaumba, na tukavitia nguvu viungo vyao. Na tukitaka tutawabadilisha mfano wao wawe badala yao.
- Yusuf akasema: Nifanye mshika khazina za nchi. Kwani hakika mimi ni mlinzi mjuzi.
- Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu.
- Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.
- Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu; na
- Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe.
- Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi.
- Basi hatuna waombezi.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



