Surah Maidah aya 89 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴾
[ المائدة: 89]
Mwenyezi Mungu hatakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakushikeni kwa mnavyo apa kweli kweli kwa makusudio. Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha wastani mnacho walisha ahali zenu, au kuwavisha, au kumkomboa mtumwa. Asiye pata hayo, basi afunge siku tatu. Hii ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapo apa. Na hifadhini yamini zenu. Namna hivyo Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake ili mpate kushukuru.
Surah Al-Maidah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Allah will not impose blame upon you for what is meaningless in your oaths, but He will impose blame upon you for [breaking] what you intended of oaths. So its expiation is the feeding of ten needy people from the average of that which you feed your [own] families or clothing them or the freeing of a slave. But whoever cannot find [or afford it] - then a fast of three days [is required]. That is the expiation for oaths when you have sworn. But guard your oaths. Thus does Allah make clear to you His verses that you may be grateful.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Mwenyezi Mungu hatakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakushikeni kwa mnavyo apa kweli kweli kwa makusudio. Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha wastani mnacho walisha ahali zenu, au kuwavisha, au kumkomboa mtumwa. Asiye pata hayo, basi afunge siku tatu. Hii ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapo apa. Na hifadhini yamini zenu. Namna hivyo Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake ili mpate kushukuru.
Mwenyezi Mungu hakutiini adabu kwa sababu ya kuapa kiapo msicho kusudia. Bali hakika Yeye hukutieni adabu kwa sababu ya kuvunja viapo mlivyo vikusudia na yamini mliyo jifunga nayo. Basi ikiwa mmevunja kiapo itakupaseni mfanye jambo la kukughufirieni dhambi zake. Na mambo yenyewe ni: kuwalisha mafakiri kumi kwa siku moja, kwa chakula cha kawaida mnacho kila nyinyi na jamaa zenu mnao waangalia, yaani watu wenu wa nyumbani bila ya israfu wala ubakhili. Au kuwavika mafakiri kumi kwa kivazi kilicho zowewa. Au kumkomboa mtu kutoka utumwani. (Na mfano wa mtumwa ni mtu alioko kifungoni kwa dhulma, au chini ya utawala wa dhulma.) Ikiwa mwenye kuapa hawezi kutenda lolote katika hayo, basi itampasa afunge siku tatu. Na kila moja katika mambo haya hufuta dhambi za mwenye kuapa kiapo cha kutilia niya na akakivunja. Nanyi zilindeni yamini zenu, msiape katika mambo yasiyo kuwa laiki yake, na wala msiache kutenda kitendo cha kughufiria dhambi pindi mkivunja kiapo. Kwa mpango huu Mwenyezi Mungu anakufafanulieni hukumu zake ili mpate kushukuru neema zake kwa kuzijua na kuzifuata vilivyo. Katika hukumu ya yamini pana mawili yafaa tuyazingatie. Kwanza: Uislamu umeraghibisha sana kukomboa watumwa. Sababu nyingi zinazo wajibisha hayo. Kafara nyingi za dhambi zinahitaji kukomboa. Kafara ya kula mchana Ramadhani yahitaji ukombozi, n.k. Na katika hayo yanaonyesha Uislamu unachukia utumwa. Uislamu uliukiri utumwa kwa kuwa maadui wao walikuwa wakiwatia utumwani Waislamu, basi na Uislamu ukaruhusu kuwatendea wao vivyo hivyo. Pili: Uislamu unakazania kulisha masikini kila ikipatikana fursa.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia.
- Na akasema: Enyi wanangu! Msiingie mlango mmoja, bali ingieni kwa milango mbali mbali. Wala mimi
- Hakika wewe ni miongoni mwa walio tumwa,
- Wakasema: Wallahi! Mwenyezi Mungu amekufadhilisha wewe kuliko sisi, na hakika sisi tulikuwa wenye kukosa.
- Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda.
- Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni?
- Hapo basi bila ya shaka tungeli kuonjesha adhabu mardufu ya uhai, na adhabu mardufu ya
- Mwenyezi Mungu hubadilisha usiku na mchana. Hakika katika hayo yapo mazingatio kwa wenye kuona.
- Afanyae wema atalipwa mfano wake mara kumi. na afanyae ubaya hatalipwa ila sawa nao tu.
- (Mwenyezi Mungu) anajua khiyana ya macho na yanayo ficha vifua.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Maidah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Maidah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Maidah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers