Surah Maidah aya 90 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ﴾
[ المائدة: 90]
Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.
Surah Al-Maidah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
O you who have believed, indeed, intoxicants, gambling, [sacrificing on] stone alters [to other than Allah], and divining arrows are but defilement from the work of Satan, so avoid it that you may be successful.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.
Enyi wenye kumsadiki Mwenyezi Mungu na Vitabu vyake na Mitume wake, wenye kuifuata Haki! Kunywa au kuvuta chochote kinacho lewesha, kucheza kamari, na kusimamisha mawe ya kutolea mihanga kwa ajili ya masanamu mnayo yaabudu, na kuagua kwa mishale, na mawe, na karatasi za kuagulia kudra iliyo ghaibu...yote hayo si chochote ila ni uchafu wa kiroho, na upotovu. Na hayo ni kupambiwa na Shetani tu. Basi yaachilieni mbali ili mpate kufuzu duniani kwa maisha bora, na Akhera mpate Janna yenye neema. Kuagua kwa mishale: ilikuwa ikiandikwa juu ya vijiti, kimoja kiliandikwa: -Mola wangu Mlezi kaniamuru-, na kingine:-Mola wangu Mlezi kanikataza-, na kingine hakikuandikwa kitu. Hutiwa vijiti hivyo katika mfuko kisha huchanganywa, na kohani hutia mkono wake akachomoa kimojapo, na akamjuvya mwenye kuuliza lilio aguliwa
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini.
- Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.
- Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma.
- Enyi mlio amini! Mnapo safiri katika Njia ya Mwenyezi Mungu basi hakikisheni, wala msimwambie anaye
- Sema: Mimi nakunasihini kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi
- Wakasema: Sisi hatukukukataza usimkaribishe yeyote?
- Na enyi watu wangu! Timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu wala msiwakhini watu vitu vyao;
- Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito.
- Unababua ngozi iwe nyeusi.
- Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Maidah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Maidah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Maidah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers