Surah Maidah aya 91 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُوقِعَ بَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّهِ وَعَنِ الصَّلَاةِ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّنتَهُونَ﴾
[ المائدة: 91]
Hakika Shet'ani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha?
Surah Al-Maidah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Satan only wants to cause between you animosity and hatred through intoxicants and gambling and to avert you from the remembrance of Allah and from prayer. So will you not desist?
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Hakika Shetani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kwa ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha?
Bila ya shaka Shetani hana atakalo kwa kukushawishini kunywa ulevi na kucheza kamari ila kuleta khitilafu na ugomvi na kuchukiana baina yenu ili mdhoofike kwa kuondoka masikizano, na uvunjike umoja wenu, kwa sababu anavyo kukupendeleeni mnywe ulevi na mcheze kamari. Na hayo ili mpate kuacha kumuabudu Mwenyezi Mungu, na muache Swala, ili Akhera yenu iwe ovu kama ilivyo dunia yenu. Basi jee! Baada ya nyinyi kujua maovu haya hamyatupilii mbali ninayo kukutazeni, mkamkosesha Iblisi makusudio yake? Mwenyezi Mungu Mtukufu Aliye takasika ametaja mambo mane yaliyo pelekea kuharimishwa ulevi na kamari: La Kwanza - Kuwa nafsi yake ni uchafu na uovu, kwani hayumkiniki kusifika kuwa ni mambo mazuri, kwa kuwa madhara yake yanaonekana wazi. Katika ulevi kuna uharibifu wa akili, na katika kamari ni kupoteza mali, na kwa yote mawili hayo upo uharibifu wa moyo. Na Shetani ndiye mwenye kuyapamba hayo. La pili - Hayo hueneza uadui na chuki. Kamari humalizikia ugomvi, na kama haifikii hayo basi huleta chuki na bughdha. Na ulevi ndio Mama wa Maasi. Utamwona mtu mwenye adabu zake mpole, akisha kunywa hugeuka nyama mwitu, akatenda mambo ya ukhalifu, kwani ulevi huidhoofisha sauti ya utu inayo mkataza mwanaadamu kutenda maovu. Utamwona mtu anajizuia kufanya kitendo kiovu, lakini akisha kunywa ulevi, au akavuta bangi, japo kidogo, huiendea shari bila ya kujali. Basi si kama ulevi unaharibu akili tu, bali unalaza dhamiri ya mtu. Anakuwa hana junaha. La tatu: Ni kuwa kamari na ulevi huuwa moyo. Mtu huwa hamkumbuki Mwenyezi Mungu, na kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndiko kunako huisha nyoyo. Lane: Maasi hayo yanamzuilia mtu na Swala. Kamari na ulevi humsahaulisha Muumini na Swala zake, na akiwa anasali hatimizi nguzo zake kama zitakikanavyo. Basi inakuwa Swala zake ni kuinama na kuinuka bila ya kufuatana na moyo. Kwa hivyo basi imethibiti kuwa kuharimishwa mvinyo, pombe, tembo, bangi n.k. si kwa sababu ya kulevya kwake tu, bali ni kwa kumziba mtu fahamu zake, kumgubika asitambue atendalo. Na kwa hivyo ndio imepokewa kuwa kinacho levya kwa wingi wake, basi hata kidogo chake ni haramu, kwani hicho kidogo nacho kinapumbaza akili. Na juu ya haya pana madhara ya mwili kama madaktari walivyo thibitisha. Kwa hivyo ulevi hata kidogo ni haramu. Mwenyezi Mungu Subhanahu ametaja sababu mbili za kuharimisha ulevi, na udaktari umezidisha kuwa ulevi kidogo haupotezi akili, lakini huzidisha uchangamfu au husabibisha hali ya huzuni na kuona dhiki ya moyo. Na katika hali zote mbili anakuwa mtu amepungukiwa na ukamilifu wa akili yake kubeba jukumu, na kwa hivyo hutenda vitendo ambavyo kwa dhahiri ni sawa kumbe ni madhara. Ama kuuzoea ulevi hudhuru maini, matumbo, na mishipa ya akili na hisiya, na hurithisha madhara mpaka kwa vizazi.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu!
- Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.
- Nasi tutawaita Mazabania!
- Na wengi wao hawafuati ila dhana tu. Na dhana haifai kitu mbele ya haki. Hakika
- Je! Mnabishana naye kwa aliyo yaona?
- Na hakika walikaribia kukushawishi uache tuliyo kufunulia ili utuzulie mengineyo. Na hapo ndio wangeli kufanya
- Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa,
- Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu; basi nisamehe. Akamsamehe; hakika Yeye ni
- Nao huwazuia watu, na wao wenyewe wanajitenga nayo. Nao hawaangamizi ila nafsi zao tu, wala
- Na hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako. Na mtakuja ulizwa.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Maidah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Maidah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Maidah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers