La sourate Al-Mutaffifin en Swahili
وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ(1) Ole wao hao wapunjao! |
الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُوا عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ(2) Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe. |
وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ(3) Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza. |
أَلَا يَظُنُّ أُولَٰئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ(4) Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa |
لِيَوْمٍ عَظِيمٍ(5) Katika Siku iliyo kuu, |
يَوْمَ يَقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ(6) Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote? |
كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٍ(7) Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin. |
وَمَا أَدْرَاكَ مَا سِجِّينٌ(8) Unajua nini Sijjin? |
كِتَابٌ مَّرْقُومٌ(9) Kitabu kilicho andikwa. |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ(10) Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha! |
الَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ(11) Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo. |
وَمَا يُكَذِّبُ بِهِ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ(12) Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi. |
إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ(13) Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale! |
كَلَّا ۖ بَلْ ۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ(14) Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma. |
كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ(15) Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi. |
ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُو الْجَحِيمِ(16) Kisha wataingia Motoni! |
ثُمَّ يُقَالُ هَٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ(17) Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha. |
كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْأَبْرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ(18) Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin. |
وَمَا أَدْرَاكَ مَا عِلِّيُّونَ(19) Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin? |
كِتَابٌ مَّرْقُومٌ(20) Kitabu kilicho andikwa. |
يَشْهَدُهُ الْمُقَرَّبُونَ(21) Wanakishuhudia walio karibishwa. |
إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ(22) Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema. |
عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ(23) Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia. |
تَعْرِفُ فِي وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ النَّعِيمِ(24) Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema, |
يُسْقَوْنَ مِن رَّحِيقٍ مَّخْتُومٍ(25) Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri, |
خِتَامُهُ مِسْكٌ ۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ(26) Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana. |
وَمِزَاجُهُ مِن تَسْنِيمٍ(27) Na mchanganyiko wake ni Tasniim, |
عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا الْمُقَرَّبُونَ(28) Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa. |
إِنَّ الَّذِينَ أَجْرَمُوا كَانُوا مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا يَضْحَكُونَ(29) Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini. |
وَإِذَا مَرُّوا بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ(30) Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana. |
وَإِذَا انقَلَبُوا إِلَىٰ أَهْلِهِمُ انقَلَبُوا فَكِهِينَ(31) Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi. |
وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوا إِنَّ هَٰؤُلَاءِ لَضَالُّونَ(32) Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea. |
وَمَا أُرْسِلُوا عَلَيْهِمْ حَافِظِينَ(33) Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao. |
فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ(34) Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri, |
عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ(35) Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia. |
هَلْ ثُوِّبَ الْكُفَّارُ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ(36) Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda? |
Plus de sourates en Swahili :
Téléchargez la sourate avec la voix des récitants du Coran les plus célèbres :
Téléchargez le fichier mp3 de la sourate Al-Mutaffifin : choisissez le récitateur pour écouter et télécharger la sourate Al-Mutaffifin complète en haute qualité.















Donnez-nous une invitation valide