Surah Anam aya 1 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَجَعَلَ الظُّلُمَاتِ وَالنُّورَ ۖ ثُمَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ﴾
[ الأنعام: 1]
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi, na akafanya giza na mwangaza. Tena baada ya haya walio kufuru wanawafanya wengine sawa na Mola wao Mlezi.
Surah Al-Anam in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
[All] praise is [due] to Allah, who created the heavens and the earth and made the darkness and the light. Then those who disbelieve equate [others] with their Lord.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi, na akafanya giza na mwangaza. Tena baada ya haya walio kufuru wanawafanya wengine sawa na Mola wao Mlezi.
Kuhimidiwa, yaani kusifiwa na kutajwa kwa wema, ni kwa Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi, na akaumba, kwa kudra yake, giza na mwangaza, kwa manufaa ya waja wake, na kuambatana na hikima yake. Tena pamoja na neema zote hizi nzuri hawa makafiri wanakwenda mshirikisha Mwenyezi Mungu, na wakawafanya wengineo ni washirika wa Mwenyezi Mungu katika ibada!! Aya hii tukufu ni ishara ya ubora wa kuumba, na ubora wa kuumba unaonyesha Umoja na Upweke wa Mwenye kuumba na utukufu wake. Kwani mbingu na nyota zake, na sayari zake, na jua, na mwezi - vyote hivyo ni ushahidi wa Umoja wake. Na ardhi na viliomo ndani yake, navyo ni wanyama, mimea na visio na uhai, na milima na mabonde, na rutuba na ukame, na viliomo chini ya ardhi maadeni magumu na yanayo tiririka, na bahari na viliomo ndani yake kama lulu na vilio hai - vyote hivyo vinaonyesha Umoja wa Mwenye kuumba. Na giza la kila namna, kama giza la jabali, na bahari, na mapango, na ukungu ulio funga moja kwa moja hata mtu akiutoa mkono wake anakaribia kuwa asiouone - pia vyote hivyo vinaonyesha ujuzi usio kuwa na mfano, wa kuanzisha kuumba, wa Mwenyezi Mungu Aliye viumba. Hali kadhaalika nuru, na sababu zake mbali mbali, kama nuru ya jua, na mwangaza wa mwezi, na mwangaza wa nyota ... vyote hivyo vinaonyesha uanzishaji wa Mwenyezi Mungu wa kuumba bila ya kiigizo.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee rehema. Hakika maombi yako
- Kwani hawawaoni ndege walioko juu yao namna wanavyo zikunjua mbawa zao, na kuzikunja? Hawawashikilii ila
- Kaf Ha Ya A'yn S'ad
- Kwa hakika wanaume wanao toa sadaka, na wanawake wanao toa sadaka, na wakamkopesha Mwenyezi Mungu
- Na pia kwa kufuru zao na kumsingizia kwao Maryamu uwongo mkubwa,
- Enyi mlio amini! Mnapo nong'ona msinong'one kwa sababu ya mambo ya madhambi, na uadui, na
- Na anapo tajwa Mwenyezi Mungu peke yake nyoyo za wasio iamini Akhera huchafuka. Na wanapo
- Na huwaje wakufanye wewe hakimu nao wanayo Taurati yenye hukumu za Mwenyezi Mungu? Kisha baada
- Akasema: Yeye anasema: Kuwa huyo ni ng'ombe asiye tiwa kazini kulima ardhi wala kumwagia maji
- Namna hivi anakubainishieni Mwenyezi Mungu Aya zake ili mpate kufahamu.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anam with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anam mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anam Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers