Surah Nisa aya 171 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ وَلَا تَقُولُوا عَلَى اللَّهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ إِنَّمَا الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ اللَّهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَىٰ مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِّنْهُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّهِ وَرُسُلِهِ ۖ وَلَا تَقُولُوا ثَلَاثَةٌ ۚ انتَهُوا خَيْرًا لَّكُمْ ۚ إِنَّمَا اللَّهُ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ ۖ سُبْحَانَهُ أَن يَكُونَ لَهُ وَلَدٌ ۘ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَكَفَىٰ بِاللَّهِ وَكِيلًا﴾
[ النساء: 171]
Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha.
Surah An-Nisa in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
O People of the Scripture, do not commit excess in your religion or say about Allah except the truth. The Messiah, Jesus, the son of Mary, was but a messenger of Allah and His word which He directed to Mary and a soul [created at a command] from Him. So believe in Allah and His messengers. And do not say, "Three"; desist - it is better for you. Indeed, Allah is but one God. Exalted is He above having a son. To Him belongs whatever is in the heavens and whatever is on the earth. And sufficient is Allah as Disposer of affairs.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha.
Enyi Watu wa Kitabu! Msipindukie haki, mkazidisha kupita kiasi katika dini yenu, wala msimzulie uwongo Mwenyezi Mungu, mkaukanya utume wa Isa, au mkamfanya kuwa ni Mungu pamoja na Mwenyezi Mungu. Kwani Masihi ni Mtume kama walivyo Mitume wengine. Mwenyezi Mungu amemuumba kwa uwezo wake na neno lake alilo mbashiria kwalo, na Jibrili akampulizia Maryamu roho ya Mwenyezi Mungu. Hii ni siri katika siri za uwezo wake Mwenyezi Mungu. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake wote imani ya kweli. Wala msidai kuwa katika Ungu kuna Utatu!! Tokeni katika upotovu huu, itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu, wala hana mshirika wake. Naye ametakasika na kuwa na mwana! Na kila kilioko katika mbingu na ardhi ni chake. Na Yeye Mwenyewe anajitosha peke yake kuwa ni Mwendeshaji wa Ufalme wake. (Kuitwa Nabii Isa Neno au Roho iliyo toka kwa Mungu, hakumpi Ungu. Yeye ni neno kwa kuumbwa kwa amri ya -Kun-, -Kuwa- akawa. Haya ni kuwapinga Mayahudi walio dai kuwa yeye ni mwanaharamu. Basi wanaambiwa kuwa ameumbwa kama vilivyo umbwa vitu vyote, kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Naye ni Roho iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu kama walivyo pewa Waumini wote (58.22) na alivyo puliziwa Adam (15.29) na kwa hivyo wanaadamu wote (32.7-9). Hapana hata pahala pamoja katika Injili ziliomo katika Biblia ambapo Yesu (Nabii Isa a.s.) alijiita mwenyewe Mwana wa Mungu. Kila mara akijiita Mwana wa Adamu. Na alipo mwita Mungu Baba, alikusudia ni Baba wa watu wote, kama alipo sema: -Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.- Injili ya Yohana 10.33-36.)
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- (Musa) akasema: Usinichukulie kwa niliyo sahau, wala usinipe uzito kwa jambo langu.
- Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni?
- Sema: Nyinyi hamtaulizwa kwa makosa tuliyo yafanya, wala sisi hatutaulizwa kwa mnayo yatenda nyinyi.
- Katika Bustani zenye neema.
- Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukanya
- Basi walikwenda na huku wakinong'onezana,
- Na wakasema: Sisi tuna mali mengi zaidi na watoto, wala sisi hatutaadhibiwa.
- Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya
- Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo?
- Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nisa with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nisa mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nisa Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers