Surah Raad aya 41 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا نَأْتِي الْأَرْضَ نَنقُصُهَا مِنْ أَطْرَافِهَا ۚ وَاللَّهُ يَحْكُمُ لَا مُعَقِّبَ لِحُكْمِهِ ۚ وَهُوَ سَرِيعُ الْحِسَابِ﴾
[ الرعد: 41]
Je! Hawakuona kwamba tunaifikia ardhi tukiipunguza nchani mwake? Na Mwenyezi Mungu huhukumu, na hapana wa kupinga hukumu yake, naye ni Mwepesi wa kuhisabu.
Surah Ar-Rad in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Have they not seen that We set upon the land, reducing it from its borders? And Allah decides; there is no adjuster of His decision. And He is swift in account.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Je! Hawakuona kwamba tunaifikia ardhi tukiipunguza nchani mwake? Na Mwenyezi Mungu huhukumu, na hapana wa kupinga hukumu yake, naye ni Mwepesi wa kuhisabu.
Na hakika dalili za adhabu na kushindwa zipo! Hawaangalii kwamba Sisi tunazifikia nchi walizo kuwa wakizitawala zinachukuliwa na Waumini kidogo kidogo? Na kwa hivyo tunawapunguzia wao ardhi zilio wazunguka. Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye wa kuhukumu kushinda na kushindwa, na thawabu na adhabu. Na wala hapana wa kuipinga hukumu yake. Na hisabu yake ni ya mbio mbio, haihitajii kupitiwa na wakati mrefu, kwani Yeye ni Mjuzi wa kila kitu. Basi ishara zipo! Aya hii ina ukweli ulio fikiliwa na uchunguzi wa kisayansi za hivi sasa, ya kwamba imethibiti kuwa dunia inazunguka, na kuwa inayo mvuto kama simaku. Hayo yamepelekea kubabataa katika ncha mbili za kaskazini na kusini, North Pole na South Pole. Na hivyo ni kupunguka katika ncha mbili za ardhi. Na kadhaalika imejuulikana kuchopoka mbio za sehemu za gasi zilizo funika huu mpira wa dunia kukipindukia nguvu za mvuto wa ardhi, basi hutoka nje ya dunia. Na haya yanatokea mfululizo, na kwa hivyo ardhi, yaani dunia, inakuwa katika hali ya kupunguka moja kwa moja katika ncha zake. Haya yanakuwa kwa kuifasiri ardhi kuwa ni dunia, si nchi ya maadui wa Waumini. Yaelekea taf siri hii kwa Aya hii tukufu, ijapo kuwa wafasiri wengi wamefasiri kuwa muradi wa -ardhi- ni nchi za maadui.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo vifanya!
- Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi
- Kila chakula kilikuwa halali kwa Wana wa Israili isipo kuwa alicho jizuilia Israili mwenyewe kabla
- Wala nisingeli jua nini hisabu yangu.
- Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Basi waachilie mbali,
- Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
- Na inapo teremshwa Sura isemayo: Muaminini Mwenyezi Mungu na piganeni Jihadi pamoja na Mtume wake,
- Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa walio rogwa.
- Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati wapate kusaidiwa!
- Na akaingia mjini wakati wa kughafilika wenyeji wake, na akakuta humo watu wawili wanapigana -
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Raad with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Raad mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Raad Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers