Surah Zumar aya 5 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ يُكَوِّرُ اللَّيْلَ عَلَى النَّهَارِ وَيُكَوِّرُ النَّهَارَ عَلَى اللَّيْلِ ۖ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۗ أَلَا هُوَ الْعَزِيزُ الْغَفَّارُ﴾
[ الزمر: 5]
Ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Hufunika usiku juu ya mchana, na hufunika mchana juu ya usiku. Na amefanya jua na mwezi vitumike. Kila kimojapo kinakwenda kwa kipindi kilicho wekewa. Jueni mtanabahi! Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe!
Surah Az-Zumar in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
He created the heavens and earth in truth. He wraps the night over the day and wraps the day over the night and has subjected the sun and the moon, each running [its course] for a specified term. Unquestionably, He is the Exalted in Might, the Perpetual Forgiver.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Hufunika usiku juu ya mchana, na hufunika mchana juu ya usiku. Na amefanya jua na mwezi vitumike. Kila kimojapo kinakwenda kwa kipindi kilicho wekewa. Jueni mtanabahi! Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe!
Ameumba mbingu na ardhi kwa kushikamana na Haki na kuwa sawa kwa kufuatana na sharia zilizo thibiti. Usiku unaufunika mchana, na mchana unaufunika usiku kwa mfululizo. Na amedhalilisha jua na mwezi kwa mujibu atakavyo na kwa mujibu wa maslaha ya waja wake. Kila kimojapo katika hivyo vinakwenda katika njia yake mpaka ufike wakati aliyo uwekea Yeye, nao ni Siku ya Kiyama. Jueni basi kuwa Yeye tu, si mwenginewe, ndiye Mwenye kushinda kila kitu. Basi hapana kitu chochote kilicho tokana na atakavyo Yeye, ambaye amefikilia ukomo wa kuwasamehe wenye kutenda madhambi katika waja wake. Aya hii tukufu inaonyesha kuwa ardhi ina sura ya mviringo kama mpira, na inazunguka wenyewe kwa wenyewe juu ya msumari-kati wake. Kwani kule kutumiwa neno Yukawwiru katika Kiarabu na ikafasiriwa Hufunika, maana yake ni kufunika kitu kwa kitu kwa namna ya kufuatana, kukariri, mara kwa mara. Na lau kuwa ardhi haina sura ya mpira, kwa mfano kuwa batabata tu, usiku ungeli enea kote kwa ghafla, au mchana ungeli angaza dunia nzima kwa mara moja.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na matunda, na malisho ya wanyama;
- Na kwa Nyumba iliyo jengwa,
- Je! Hawakuona kwamba tunaifikia ardhi tukiipunguza nchani mwake? Na Mwenyezi Mungu huhukumu, na hapana wa
- Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi,
- Je! Yule aliye pambiwa a'mali zake mbaya na akaziona ni njema - basi hakika Mwenyezi
- Siku hiyo Mwenyezi Mungu atawapa sawa sawa malipo yao ya haki, na watajua kwamba hakika
- Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyume na hivyo. Tumekuwa
- Hayo ni kwa sababu waliyachukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao.
- Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli.
- Akasema: Enyi wahishimiwa! Ni nani kati yenu atakaye niletea kiti chake cha enzi kabla hawajanijia
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Zumar with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Zumar mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Zumar Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers