Surah Qasas aya 57 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَقَالُوا إِن نَّتَّبِعِ الْهُدَىٰ مَعَكَ نُتَخَطَّفْ مِنْ أَرْضِنَا ۚ أَوَلَمْ نُمَكِّن لَّهُمْ حَرَمًا آمِنًا يُجْبَىٰ إِلَيْهِ ثَمَرَاتُ كُلِّ شَيْءٍ رِّزْقًا مِّن لَّدُنَّا وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴾
[ القصص: 57]
Na wakasema: Tukiufuata uwongofu huu pamoja nawe tutanyakuliwa kutoka nchi yetu. Je! Kwani Sisi hatukuwaweka imara katika pahala patakatifu, penye amani, ambapo huletewa matunda ya kila aina kuwa ni riziki itokayo kwetu? Lakini wengi wao hawajui.
Surah Al-Qasas in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And they say, "If we were to follow the guidance with you, we would be swept from our land." Have we not established for them a safe sanctuary to which are brought the fruits of all things as provision from Us? But most of them do not know.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na wakasema: Tukiufuata uwongofu huu pamoja nawe tutanyakuliwa kutoka nchi yetu. Je! Kwani Sisi hatukuwaweka imara katika pahala patakatifu, penye amani, ambapo huletewa matunda ya kila aina kuwa ni riziki itokayo kwetu? Lakini wengi wao hawajui.
Na washirikina wa Makka walimwambia Mtume s.a.w. kwa kujitolea udhuru kwa kubakia kwao katika dini yao: Tukikufuata wewe katika dini yako Waarabu watatutoa katika nchi yetu, na watatushinda katika utawala wetu. Na hakika wao ni waongo katika kutoa udhuru wao huo. Kwani Mwenyezi Mungu alikuwa kawaweka imara na madhubuti katika nchi yao. Na akaifanya nchi takatifu yenye amani, hawashambuliwi wala hawauwawi, na hali wao ni makafiri. Na wanaletewa matunda na kheri nyengine za aina nyingi, ambazo Mwenyezi Mungu anawaletea kutoka kila upande. Basi huwaje awaondolee amani, na awaachilie wakinyakuliwa wakiongeza juu ya utakatifu wa Nyumba ya Alkaaba Imani kumuamini Muhammmad! Lakini wengi wao hawaijui Haki. Lau kuwa wanaijua wasinge khofu kunyakuliwa.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Aliye kujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha.
- Hakika mimi nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wangu na Mola Mlezi wenu. Hapana kiumbe yeyote
- Je! Yule mwenye kustahiki hukumu ya adhabu, je, wewe unaweza kumwokoa aliyomo katika Moto?
- Enyi mlio amini! Msizifuate nyayo za Shet'ani. Na atakaye fuata nyayo za Shet'ani basi yeye
- Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem,
- Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini.
- Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na
- Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisio tambaa, na
- Siku tutayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa.
- Akaitupa. Mara ikawa nyoka anaye kwenda mbio.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Qasas with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Qasas mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Qasas Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers