Surah Tawbah aya 60 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿۞ إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ﴾
[ التوبة: 60]
Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni waajibu ulio faridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima.
Surah At-Tawbah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Zakah expenditures are only for the poor and for the needy and for those employed to collect [zakah] and for bringing hearts together [for Islam] and for freeing captives [or slaves] and for those in debt and for the cause of Allah and for the [stranded] traveler - an obligation [imposed] by Allah. And Allah is Knowing and Wise.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni waajibu ulio faridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima.
Zaka iliyo faridhiwa haitumiwi ila kwa mafakiri wasio pata cha kuwatosha, na masikini wagonjwa ambao hawawezi kazi wala hawana mali, na wale wanao itumikia kwa kuikusanya, na wanao tiwa moyo kwa sababu wanatarajiwa kusilimu na kupatikana kwao manufaa kwa utumishi wao na kuunusuru Uislamu, na wale wanao eneza Uislamu na kufanya tabshiri (Daawa), na katika kuwakomboa waliomo utumwani na walio tekwa, na kuwatoa waliomo katika unyonge na utawala wa madhila, na katika kuwalipia wenye madeni walio shindwa kuyalipa ikiwa hayo madeni hayakutokana na madhambi au dhulma au upumbavu, na katika kuzatiti Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na katika mambo kama hayo yaliyomo katika njia za kheri na wema, na katika kusaidia wasafiri walio katikiwa kupata msaada wa mali yao na watu wao. Mwenyezi Mungu ameyatungia sharia hayo kuwa ni waajibu kwa ajili ya maslaha ya waja wake. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Mwenye kujua vyema maslaha ya viumbe vyake, na Mwenye hikima kwa anayo yafanyia sharia. Zaka ni mpango ulio wekwa wa kukusanya mali kutokana na matajiri na kurudishiwa mafakiri. Kwa hivyo ni haki ya mafakiri katika mali ya matajiri. Na huyakusanya mtawala na huyatumilia kwa njia zake ambazo zinahisabiwa kuwa ndio muhimu kabisa na bora hizo ni kupiga vita athari za ufakiri kwa mafakiri. Hupewa mafakiri, masikini, wasafiri, kusaidiwa mwenye deni aliye kopa kwa jambo la halali si kwa uharibifu, na katika hayo ipo njia ya kupewa mkopo -kardhan hasanan- (mkopo kwa Lillahi). Katika mwanzo wa Uislamu ilivyo kuwa Zaka inatozwa na kutumiwa vilivyo hapakuwapo katika umma mtu anaye lala na njaa, wala mwombaji aliye dhalilika kwa haja. Ilifika hadi hata wenye kutumikia Zaka wakashitaki kuwa jinsi ya kuenea neema hapana wa kustahiki kupewa. Alishitaki mmoja wapo katika Afrika kumshitakia Khalifa Umar bin Abdulaziz kuwa hakumpata fakiri wa kumpa Zaka. Umar akamwambia walipie wenye madeni. Akawalipia. Bado akashitaki tena. Akamwambia wanunue watumwa uwape uhuru wao. Huo basi ndio utumiwaji wa Zaka. Na ukitaka kweli, ni kuwa lau kuwa Zaka zikikusanywa kwa inavyo faa, na zikatumiliwa zinavyo stahiki basi huo bila ya shaka ungeli kuwa ni mpango bora kabisa wa kudhamini maisha ya umma yasipate shida ya umasikini.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hakika Sisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali.
- Lakini aliye dhulumu, kisha akabadilisha wema baada ya ubaya, basi Mimi ni Mwenye kusamehe Mwenye
- Au ikasema inapo ona adhabu: Lau kuwa ningeli pata fursa nyengine, ningeli kuwa miongoni mwa
- Na wanapo kumbushwa hawakumbuki.
- Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno
- Hakika katika hayo zipo ishara kwa waaguzi.
- Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi na tukayatuliza katika ardhi. Na hakika Sisi tunaweza
- Siku atapo wafufua Mwenyezi Mungu, na awaambie yale waliyo yatenda. Mwenyezi Mungu ameyadhibiti, na wao
- Kwa hakika wanao rudi nyuma baada ya kwisha wabainikia uwongofu, Shetani huyo amewashawishi na amewaghuri.
- Bila ya shaka wanao fungamana nawe, kwa hakika wanafungamana na Mwenyezi Mungu. Mkono wa Mwenyezi
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Tawbah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Tawbah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Tawbah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers