Surah Waqiah aya 6 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿فَكَانَتْ هَبَاءً مُّنبَثًّا﴾
[ الواقعة: 6]
Iwe mavumbi yanayo peperushwa,
Surah Al-Waqiah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And become dust dispersing.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Iwe mavumbi yanayo peperushwa!
Ikawa vumbi la kupeperushwa, Aya hizi tukufu zinaeleza hadi gani vitakuwa vitisho vitavyo uteremkia ulimwengu kitapo fika Kiyama. Na katika vitisho hivyo ni hayo masaibu ya dunia yatakayo athiri ardhi na matabaka yake. Kwani hii ardhi tunayo ishi juu ya mgongo wake si yenye kutulia na kukaa sawa kwa utimilivu. Kwani hiyo imeundwa kwa matabaka ya majabali yaliyo ingiliana ovyo. Huenda baadhi yao yakateremka yakaachana na mengineyo yaliyo jirani nayo. Na huwa hiyo inayo itwa kupasuka kwa matabaka ya ardhi, Geological cleavage kama inavyo tokea katika maeneo kadhaa wa kadhaa. Mpasuko huu ulikuwa na ungali kuwa ndio asili ya chini kabisa ya zilzala, mitetemeko, mikubwa kwa kuathirika na nguvu za kudidimiza na kuvuta zinazo fuatana na matabaka ya ardhi yanapo vunjika. Basi mizani ya utulivu ya nguvu hizi inapo geuka kwa kuathirika na mambo mengineyo ya nje huenda zikafunguka nguvu za mtikiso mkubwa ndio ikatokea mitetemeko na mitikisiko ya ardhi, ambayo hubomoa kila kitu kiliopo juu ya ardhi karibu na ilipo anzia hiyo zilzala. Na hapo tena hutokea uharibifu mkubwa mno. Na hayo maelezo ya kisayansi hayageuzi kitu, wala hayako mbali na nadhari ya kidini. Kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu huenda akajaalia sababu za maumbile za kawaida zikajumuika kwa njia tusiyo izoea sisi ili zikiingiliana kwa njia ya kutisha ndio sababu ya kuharibika dunia. Hapo maelezo ya kisayansi yanafuatana na Aya zenye kuonya kwa vitisho hivyo vikuu. Na yote hayo yanatokana kwa Mwenyezi Mungu. Na hutokea kwa idhini yake Mwenyezi Mungu kutimiza hukumu yake katika dunia yetu.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Yeye hakika amewadhibiti na amewahisabu sawa sawa.
- Na ndugu zao wanawavutia kwenye upotofu, kisha wao hawaachi.
- Na lau kuwa miti yote iliyomo duniani ikawa ni kalamu, na bahari (ikawa wino), na
- Enyi watu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu. Ati yupo muumba mwengine asiye kuwa
- Basi usiwe na shaka juu ya wanayo yaabudu hao. Hawaabudu ila kama walivyo abudu baba
- Na katika Ishara zake ni vyombo vinavyo kwenda na kurejea baharini kama vilima.
- Na kipofu na mwenye kuona hawalingani.
- Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote.
- Na hakika tumeisahilisha Qur'ani kuikumbuka. Lakini yupo anaye kumbuka?
- Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Waqiah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Waqiah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Waqiah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



