Surah Tawbah aya 61 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَمِنْهُمُ الَّذِينَ يُؤْذُونَ النَّبِيَّ وَيَقُولُونَ هُوَ أُذُنٌ ۚ قُلْ أُذُنُ خَيْرٍ لَّكُمْ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَيُؤْمِنُ لِلْمُؤْمِنِينَ وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ ۚ وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ رَسُولَ اللَّهِ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴾
[ التوبة: 61]
Na miongoni mwao wapo wanao muudhi Nabii na kusema: Yeye huyu ni sikio tu. Sema: Basi ni sikio la kheri kwenu. Anamuamini Mwenyezi Mungu, na ana imani na Waumini, naye ni rehema kwa wanao amini miongoni mwenu. Na wanao muudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu watapata adhabu chungu.
Surah At-Tawbah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And among them are those who abuse the Prophet and say, "He is an ear." Say, "[It is] an ear of goodness for you that believes in Allah and believes the believers and [is] a mercy to those who believe among you." And those who abuse the Messenger of Allah - for them is a painful punishment.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na miongoni mwao wapo wanao muudhi Nabii na kusema: Yeye huyu ni sikio tu. Sema: Basi ni sikio la kheri kwenu. Anamuamini Mwenyezi Mungu, na ana imani na Waumini, naye ni rehema kwa wanao amini miongoni mwenu. Na wanao muudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu watapata adhabu chungu.
Na wapo watu wanaafiki wanakusudia kumuudhi Nabii, na kumletea ya kumkirihi. Wao humtuhumu kuwa anapenda kusikiliza kila analo ambiwa, kweli na uwongo, na kwamba yeye anakhadaika na hayo anayo yasikia. Basi, ewe Mtume! Waambie: Huyo mnaye msengenya nyuma yake sio kama mnavyo dai. Bali yeye ni sikio la kheri kwenu. Hasikii ila la kweli, wala hakhadaiki na upotovu. Anamsadiki Mwenyezi Mungu na wahyi (ufunuo) wake, na anawasadiki Waumini, kwa sababu Imani yao inawakataza uwongo. Na yeye ni rehema kwa kila mmoja wenu anaye amini. Na hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia wanao muudhi Mtume adhabu chungu, na kali, na ya kudumu milele.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Kadhaalika; na tukawarithisha hayo Wana wa Israili.
- Wala msiliane mali zenu kwa baat'ili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya
- Enyi mlio amini! Msiharimishe vizuri alivyo kuhalalishieni Mwenyezi Mungu, wala msikiuke mipaka. Hakika Mwenyezi Mungu
- Sema: Haviwi sawa viovu na vyema ujapo kupendeza wingi wa viovu. Basi mcheni Mwenyezi Mungu,
- Wakamjia kaumu yake mbio mbio. Na kabla ya haya walikuwa wakitenda maovu. Yeye akasema: Enyi
- Basi nawacheke kidogo; watalia sana. Hayo ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyachuma.
- Na walikuja wenye kutoa udhuru katika Mabedui ili wapewe ruhusa, na wakakaa wale walio mwambia
- Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kaamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha. Na
- Ambao wanajionyesha,
- Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Tawbah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Tawbah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Tawbah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



