Surah Araf aya 65 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿۞ وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُ ۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ﴾
[ الأعراف: 65]
Na kwa A'adi tulimpeleka ndugu yao, Hud. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu ila Yeye. Basi je, hamumchi?
Surah Al-Araf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And to the 'Aad [We sent] their brother Hud. He said, "O my people, worship Allah; you have no deity other than Him. Then will you not fear Him?"
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na kwa aadi tulimpeleka ndugu yao, Huud. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu ila Yeye. Basi je, hamumchi?
Kama tulivyo mtuma Nuhu kwa kaumu yake kuwalingania Tawhidi, kadhaalika tuliwatumia kinaAad Nabii Huud,naye ni mmoja wao, makhusiano yake nao ni kama ndugu kwa ndugu. Akawaambia: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake, nanyi hamna Mungu asiye kuwa Yeye. Na hii ndiyo njia ya kujikinga na shari na adhabu. Nayo ndiyo Njia Iliyo Nyooka. Basi je, mtaifuata njia mjikinge na shari na upotovu?Aad ni katika kabila yenye nguvu katika matumbo ya Taifa la Sam, na ni katika matabaka ya kwanza katika Waarabu wa jangwani. Ama makaazi yao yalikuwa katika Al-ahqaaf iliyo tajwa katika Kitabu kitukufu katika Sura ya Al-ahqaaf Aya 21. Wamewafikiana wanachuoni wa Kiislamu wa kutegemewa kuwa hiyo Ahqaaf ipo katika nchi ya Yaman, ijapo kuwa wamekhitalifiana kidogo wapi khasa pahala penyewe. Kwa mujibu wa Yaaqut Al-Hamawy ni bonde baina ya Oman na nchi ya Mahara. Na kwa mujibu wa Is-haaq akimnukulu Ibn Abbas na Ibn Khaldun ni sehemu ya mchanga baina ya Oman na Hadhramaut. Kwa mujibu wa Qutaada ni sehemu ya mchanga karibu na bahari katika Shajar katika nchi ya Yaman. Na yafaa kutaja kuwa nchi yaAad kwa mujibu wa baadhi ya Wamagharibi wa zamani ipo pande za juu za Hijaz katika jimbo la Husmaa, na karibu na makaazi ya Thamud. Vyo vyote ilivyo si mbali kuwa hao kaumu yaAad walisafiri wakahamia jimbo hili wakati mmoja wapo.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini.
- Na Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa watu wawili. Mmoja wao ni bubu, hawezi chochote, naye
- Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu, na masanamu, na madeste makubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa
- Bali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao, na wakasema makafiri: Hili ni jambo la
- Wanakuapieni Mwenyezi Mungu ili kukuridhisheni nyinyi, hali ya kuwa wanao stahiki zaidi kuridhishwa ni Mwenyezi
- Akaitupa. Mara ikawa nyoka anaye kwenda mbio.
- Wakasema: Tuombee kwa Mola wako atupambanulie nini rangi yake? Akasema: Yeye anasema, kuwa ng'ombe huyo
- (Akaambiwa): Ewe Ibrahim! Wachilia mbali haya! Kwa hakika amri ya Mola wako Mlezi imekwisha kuja,
- Na hilo si gumu kwa Mwenyezi Mungu.
- Na wawili katika ngamia, na wawili katika ng'ombe. Sema: Je, ameharimisha yote madume wawili au
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Araf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Araf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Araf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers