Surah Nahl aya 69 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿ثُمَّ كُلِي مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ فَاسْلُكِي سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلًا ۚ يَخْرُجُ مِن بُطُونِهَا شَرَابٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ فِيهِ شِفَاءٌ لِّلنَّاسِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴾
[ النحل: 69]
Kisha kula katika kila matunda, na upite katika njia za Mola wako Mlezi zilizo fanywa nyepesi kuzipita. Na kutoka matumbo yao kinatoka kinywaji chenye rangi mbali mbali; ndani yake kina matibabu kwa wanaadamu. Hakika katika haya ipo Ishara kwa watu wanao fikiri.
Surah An-Nahl in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Then eat from all the fruits and follow the ways of your Lord laid down [for you]." There emerges from their bellies a drink, varying in colors, in which there is healing for people. Indeed in that is a sign for a people who give thought.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Kisha kula katika kila matunda, na upite katika njia za Mola wako Mlezi zilizo fanywa nyepesi kuzipita. Na kutoka matumbo yao kinatoka kinywaji chenye rangi mbali mbali; ndani yake kina matibabu kwa wanaadamu.Hakika katika haya ipo Ishara kwa watu wanao fikiri.
Kisha Subhanahu akamhidi Nyuki ale matunda ya miti na mimea mbali mbali, na akamsahilishia afuate njia alizo mtengezea Mola wake Mlezi, na akatoa kutokana na matumbo yake kinywaji, nacho ni asali, chenye rangi mbali mbali. Na hiyo asali imekuwa ni dawa ya kuwaponyesha watu. Hakika katika hayo pana ufundi wa ajabu wa kuonyesha nguvu, na kuwepo Mwenye kuumba, na Mwenye kuweza, Mwenye hikima. Wenye kutumia akili zao wananufaika kwa mazingatio hayo, na watapata furaha ya daima. Asali ya nyuki ni mchanganyiko wa glucose na livulose, nayo ni namna ya sukari ambayo ni nyepesi kabisa kutumika mwilini, na madaktari wamevumbua karibu kuwa glucose ina faida kutibu maradhi mengi, kwa kupiga sindano, na kwa mdomo na kwa nyuma, kwa kuwa inatia nguvu, na inapinga sumu ya maadeni kadhaa wa kadhaa, na sumu inayo patikana kwa maradhi ya viungo, kama kuingia sumu kwa mkojo na maradhi ya kuwa manjano jaundice na mengineyo. Vile vile imethibiti kuwa Vitamin nyingi hupatikana humo, na khasa Vitamin B complex.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Basi nawacheke kidogo; watalia sana. Hayo ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyachuma.
- Na kwa Madyana tulimtuma ndugu yao Shuaibu, naye akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu
- Na tutayaendea yale waliyo yatenda katika vitendo vyao, tuvifanye kama mavumbi yaliyo tawanyika.
- Na tukawarithisha watu walio kuwa wanadharauliwa mashariki na magharibi ya ardhi tuliyo ibariki. Na likatimia
- Na hakika tulikwisha kufanyia hisani mara nyengine...
- Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?
- Unao babua ngozi ya kichwa!
- Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa
- Na umshirikishe katika kazi yangu.
- Mwenyezi Mungu Mkusudiwa.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nahl with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nahl mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nahl Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers