Surah Fatiha aya 7 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ﴾
[ الفاتحة: 7]
Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.
Surah Al-Fatihah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
The path of those upon whom You have bestowed favor, not of those who have evoked [Your] anger or of those who are astray.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.
Na njia hiyo ndiyo ya waja wako ulio wawezesha kukuamini Wewe, na ukawajaalia neema ya uwongofu na radhi, sio njia ya walio stahiki kupata ghadhabu zako na wakaiwacha njia ya haki na kheri, kwa sababu hao wameitupa imani kukuamini Wewe na kuelekea kwenye uwongofu wako. (Hapana katika Vitabu vyote vitakatifu, vya dini zote, dua inayo lingana na hii kwa uzuri wake, na utimilivu wake. Baada ya kumsifu Mwenyezi Mungu kwa Rehema yake isio na ukomo wala kipimo, na kumshukuru Mola Mwenye kuviumba na kuviangalia na kuvilea kwa huruma viumbe vyote, na kuhakikisha kuwa tunajua kuwa hapana Mungu ila Yeye tu wa kuabudiwa na kuombwa msaada, na kuwa hapana wa kumuingilia katika Ufalme wake na Uwezo wake wa kulipa hisabu kwa kila alitendalo mtu, hapo tena ndio tunaomba. Na tunaomba nini? Si mkate wa kula, wala riziki yoyote, wala jambo lolote la manufaa ya kimwili duniani, bali tunaomba Uwongofu kwenye Njia Iliyo Nyooka, Njia ya kumwendea Yeye Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema. Tunaomba tusiendee njia waliyo ifuata wale walio kasirikiwa na Mwenyezi Mungu, kwa kuwa walifunzwa wakajua, lakini kwa chuki na jeuri wakakataa kuongoka, wala sio njia ya wale ambao labda kwa ujinga wamepotea. Hiyo kwa mukhtasari ndiyo Dua ambayo Waislamu, wanafunzwa waiombe, na wanaiomba mara kadhaa wa kadhaa katika Sala zao, na katika kila fursa inapo tokea.)
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na mkewe, mchukuzi wa kuni,
- Na dhara inapo mgusa mtu hutuomba. Kisha tunapo mpa neema zitokazo kwetu, husema: Nimepewa haya
- Enyi Watu wa Kitabu! Amekwisha kujieni Mtume wetu anaye kufichulieni mengi mliyo kuwa mkiyaficha katika
- Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake
- Akasema: Itupe, ewe Musa!
- Na hakika walikanushwa Mitume wa kabla yako. Nao wakavumilia kule kukanushwa, na kuudhiwa, mpaka ilipo
- Wakasema: Je! Umetujia kwa maneno ya kweli au wewe ni katika wachezao tu?
- Akasema: Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia yako Iliyo Nyooka.
- Wakasema: Bila shaka umekwisha jua hatuna haki juu ya binti zako, na unayajua tunayo yataka.
- Njia ya Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake Yeye tu viliomo mbinguni na katika ardhi. Jueni
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Fatiha with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Fatiha mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Fatiha Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers