Surah Zumar aya 7 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿إِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ اللَّهَ غَنِيٌّ عَنكُمْ ۖ وَلَا يَرْضَىٰ لِعِبَادِهِ الْكُفْرَ ۖ وَإِن تَشْكُرُوا يَرْضَهُ لَكُمْ ۗ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۗ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ۚ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴾
[ الزمر: 7]
Mkikufuru basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi, lakini hafurahii kufuru kwa waja wake. Na mkishukuru Yeye hufurahika nanyi. Wala mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi. Hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyafanya. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyomo vifuani.
Surah Az-Zumar in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
If you disbelieve - indeed, Allah is Free from need of you. And He does not approve for His servants disbelief. And if you are grateful, He approves it for you; and no bearer of burdens will bear the burden of another. Then to your Lord is your return, and He will inform you about what you used to do. Indeed, He is Knowing of that within the breasts.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Mkikufuru basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi, lakini hafurahii kufuru kwa waja wake. Na mkishukuru Yeye hufurahika nanyi. Wala mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi. Hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyafanya. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyomo vifuani.
Enyi watu! Mkizikataa neema za Mwenyezi Mungu, basi Yeye hakika si mhitaji wa imani yenu na shukrani zenu. Lakini Yeye hapendi waja wake wakufuru, kwa sababu hayo yanawadhuru wenyewe. Na mkimshukuru kwa ajili ya neema zake, Yeye huwa radhi nanyi kwa shukra hiyo. Wala mtu mwenye madhambi hayabebi madhambi ya mwenginewe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi, na hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyatenda duniani. Hakika Yeye anayajua mnayo yaficha katika nyoyo zenu ziliomo vifuani. Haya yaliomo katika Qurani Tukufu yanaweka wazi msingi wa kutoa adhabu, kama ilivyo vile vile katika Surat Yusuf katika kauli yake Mtukufu: -Akasema: Mwenyezi Mungu apishe mbali sisi kumshika yeyote ila tuliye yakuta mali yetu kwake; hivyo basi tutakuwa madhaalimu.- Na haya katika Qurani ni kusimamisha msingi ulio kwisha tajwa, nao ni msingi ambao haukuthibiti katika kanuni (sharia) za kutungwa na binaadamu ila katika zama za karibuni. (Haya ni kinyume cha ilivyo katika imani aliyo itumbukiza Paulo katika Ukristo, kwamba wanaadamu wamerithi dhambi ya Adam, wanayo ita -Dhambi ya asili-, na kwamba Nabii Isa, Yesu, kafa msalabani kwa kubeba dhambi za wanaadamu. Biblia yenyewe inapinga haya. Tazama: Jeremiah 31:29-30; Ezekieli 18 Kwa nadhariya ya Paulo Mungu amedhulumu mara mbili: 1. Kutubandika wanaadamu wote dhambi za Adam, 2. Kumbebesha -mwanawe- Yesu dhambi za walimwengu wote!)
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma
- Na sikiliza siku atapo nadi mwenye kunadi kutoka pahala karibu.
- Na mtaje katika Kitabu Ibrahim. Hakika yeye alikuwa mkweli, Nabii.
- Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya
- Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu?
- Enyi mlio amini! Ikiwa mtawat'ii walio kufuru watakurudisheni nyuma, na hapo mtageuka kuwa wenye kukhasiri.
- Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini?
- Basi wakatoka mpaka wakawafikia watu wa mji mmoja. Wakawaomba watu wake wawape chakula, nao wakakataa
- Na kwa nini tusimuamini Mwenyezi Mungu na Haki iliyo tujia, na hali tunatumai Mola wetu
- Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji?
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Zumar with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Zumar mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Zumar Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers