Surah Muminun aya 71 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَلَوِ اتَّبَعَ الْحَقُّ أَهْوَاءَهُمْ لَفَسَدَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ بَلْ أَتَيْنَاهُم بِذِكْرِهِمْ فَهُمْ عَن ذِكْرِهِم مُّعْرِضُونَ﴾
[ المؤمنون: 71]
Na lau kuwa Haki ingeli fuata matamanio yao, basi zingeli haribika mbingu na ardhi na waliomo ndani. Bali tumewaletea ukumbusho wao, nao wanajitenga mbali na ukumbusho wao.
Surah Al-Muminun in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
But if the Truth had followed their inclinations, the heavens and the earth and whoever is in them would have been ruined. Rather, We have brought them their message, but they, from their message, are turning away.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na lau kuwa Haki ingeli fuata matamanio yao, basi zingeli haribika mbingu na ardhi na waliomo ndani. Bali tumewaletea ukumbusho wao, nao wanajitenga mbali na ukumbusho wao.
Ingeli kuwa Haki inafuata matamanio yao ufisadi ungeli enea ulimwenguni, na hawa za nafsi zingeli pambana wenyewe kwa wenyewe. Lakini Sisi tumewapelekea Qurani ambayo inawakumbusha haki ambayo inapasa wote wajumuike juu yake. Na juu ya hivyo wao wanayapuuza hayo. -Na lau kuwa Haki ingeli fuata matamanio yao, basi zingeli haribika mbingu na ardhi na waliomo ndani. Bali tumewaletea ukumbusho wao, nao wanajitenga mbali na ukumbusho wao.- Hilo neno -Haki- ni tamko lenye maana kadhaa. Huweza kuwa maana yake ni -Mwenyezi Mungu- Subhanahu wa Taala , mfano wa kauli yake Mtukufu: -Ametukuka Mwenyezi Mungu wa Haki-. Pengine huwa maana yake ni -Qurani- , kwa mfano :-Hakika Sisi tumekutuma kwa Haki-. Na huenda kukusudiwa -Dini yote-, yaani miongoni mwake ni Qurani na Sunna (Hadithi) Sahihi, mfano wa kauli yake: -Na sema: Imekuja Haki na uwongo umetoweka-. Na iliyo dhaahiri katika tamko la Haki hapa ni kuwa makusudio yake ni ile maana ya kwanza, yaani -Mwenyezi Mungu- Aliye takasika na kutukuka. Na kwa hivyo maana iliyo kusudiwa na Aya ni: Lau kuwa mwenendo wa Mwenyezi Mungu unafuatana na watakayo na wanayo yapendekeza makafiri mpango usingeli bakia katika hali iliyo simamia shani ya mpango wa mbingu na ardhi na wa viumbe viliomo ndani yake. Lakini Mwenyezi Mungu Mwenye hikima kuu na uwezo wa kutenda na ujuzi wake ulio enea kwa viumbe vyake na hikima yake ikadhamini kwa mpango madhubuti, na Qurani kusema kwa uwazi ya kwamba mbingu zina viumbe, anatuelekeza tufahamu: Kwanza kuwa Kuamini hayo kwa jumla ni yakini, tuache tafsili yake mpaka apendavyo Mwenyezi Mungu Subhanahu kuidhihirisha kwa kuambatana na kauli yake: -Tutawaonyesha Ishara zetu angani na katika nafsi zao.- Pili: Anatuelekeza kwenye utafiti wa kisayansi kama tunaweza -kwani kufikilia hakika hii inatutilia nguvu Imani yetu. Na Imani ndiyo lengo muhimu katika kuelekea kwetu kwenye Ishara hizo.-
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?
- Wataelekeana wakiulizana.
- Hakika hii ndiyo riziki yetu isiyo malizika.
- Alisema: Mola wangu Mlezi anayajua yasemwayo mbinguni na katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye kusikia
- Bali ni mawaidha kwa wenye kunyenyekea.
- Tena je! Ikisha tokea mtaiamini? Je! Ndio sasa tena? Na nyinyi mlikuwa mkiihimiza.
- Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini
- Na ndiye aliye itandaza ardhi na akaweka humo milima na mito. Na katika kila matunda
- Na hichi ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa. Basi kifuateni, na mchenimngu, ili mrehemewe.
- Basi Musa akaingia khofu nafsi yake.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Muminun with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Muminun mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Muminun Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers