Surah Nahl aya 72 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَاللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنْ أَزْوَاجِكُم بَنِينَ وَحَفَدَةً وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ أَفَبِالْبَاطِلِ يُؤْمِنُونَ وَبِنِعْمَتِ اللَّهِ هُمْ يَكْفُرُونَ﴾
[ النحل: 72]
Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu, na akakujaalieni kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu, na akakuruzukuni vitu vizuri vizuri. Basi je, wanaamini upotovu na wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu?
Surah An-Nahl in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And Allah has made for you from yourselves mates and has made for you from your mates sons and grandchildren and has provided for you from the good things. Then in falsehood do they believe and in the favor of Allah they disbelieve?
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu, na akakujaalieni kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu, na akakuruzukuni vitu vizuri vizuri.Basi je, wanaamini upotovu na wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu?
Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake wa jinsi yenu mtulie nao. Tena amekupeni, kutoka kwa wake zenu, wana na wajukuu, na akakuruzukuni vitu vya kufurahisha nafsi zenu alivyo kuhalalishieni. Je, baada ya haya ndio baadhi ya watu humshirikisha Mwenyezi Mungu, na wakaamini upotovu, na wakazipinga neema za Mwenyezi Mungu zinazo onekana, ambazo zinastahiki shukrani kutoka kwao, na kumsafia ibada Mwenyezi Mungu? Ndoa ni mfungamano mtakatifu ambao ndio asili ya ukoo na kiini cha umma na jamii. Na ndoa ni mpango wa kuidhibiti ile khulka waliyo nayo wanaadamu na wanyama, nayo ni kutamani kuingiliana. Lau ingeli kuwa hapana ndoa iliyo kadiriwa kudhibiti ile khulka ya kutamaniana basi binaadamu wangeli kuwa sawa na wanyama kwa kufuata fujo na uchafu wa kuingiliana. Na hapo mwanaadamu asingeli kuwa yule kiumbe aliye mjaalia Mwenyezi Mungu kuwa na akili na fikra na akamtukuza kuliko viumbe vyengine, na akamrithisha mamlaka ya ardhi. Ilivyo kuwa mpango wa Mwenyezi Mungu katika uhai huu ni kutengeneza khulka kwa ndoa ili binaadamu awe juu kuliko wanyama wengine, hali kadhaalika binaadamu kwa upande mwengine ameumbiwa kupenda kubakia. Na ilivyo kuwa hapana njia ya kubakia yeye mwenyewe, naye anayajua hayo kutokana na baba zake na babu zake na vitu vyote vilio hai, basi njia pekee ni yeye kuzaa dhuriya wapate kuishi na kuendelea daima. Na labda lenye kuweka wazi kabisa ile khulka yake ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: -Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu, na akakujaalieni kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu, na akakuruzukuni vitu vizri vizuri.-
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na wanapo sikia upuuzi hujitenga nao na husema: Sisi tuna vitendo vyetu, na nyinyi mna
- Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi
- (Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe ni maluuni!
- Yakiwapata watu madhara humwomba Mola wao Mlezi nao wametubu kwake. Kisha akiwaonjesha rehema itokayo kwake,
- Ati kwa kuwa ana mali na watoto!
- Na hakika Harun alikwisha waambia kabla yake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmetiwa mtihanini tu
- Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari.
- Na ikiwa watarudi nyuma, basi mimi nimekwisha kufikishieni niliyo tumwa kwenu. Na Mola wangu Mlezi
- Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa
- Kisha yakawafikia waliyo kuwa wakiahidiwa,
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nahl with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nahl mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nahl Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



