Surah Baqarah aya 73 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿فَقُلْنَا اضْرِبُوهُ بِبَعْضِهَا ۚ كَذَٰلِكَ يُحْيِي اللَّهُ الْمَوْتَىٰ وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ﴾
[ البقرة: 73]
Tukasema: Mpigeni kwa kipande chake (huyo ng'ombe). Ndivyo hivi Mwenyezi Mungu huwahuisha wafu; na anakuonyesheni Ishara zake ili mpate kufahamu.
Surah Al-Baqarah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
So, We said, "Strike the slain man with part of it." Thus does Allah bring the dead to life, and He shows you His signs that you might reason.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Tukasema: Mpigeni kwa kipande chake (huyo Ngombe). Ndivyo hivi Mwenyezi Mungu huwahuisha wafu; na anakuonyesheni Ishara zake ili mpate kufahamu.
Tukakwambieni kwa ulimi wa Musa: Chukueni kipande cha nyama ya huyo Ngombe mumpige nacho, nanyi mkafanya hivyo. Mwenyezi Mungu akamfufua huyo aliye uliwa akataja jina la aliye muuwa, na kisha akafa tena. Na huo ulikuwa ni muujiza wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Musa. Kwani Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu, na kwa uwezo wake huu ndivyo anavyo huisha maiti Siku ya Kiama. Na anakuonyesheni dalili za uwezo wake ili mpate kufahamu na kuzingatia haya. Mwandishi mmoja wa zama zetu, marehemu Sh. Abdul Wahhab Annajjar ametaja kwamba kauli ya Mwenyezi Mungu: -Mpigeni kwa kipande chake- maana yake kipande cha aliye uwawa. Na makusudio ya kufufuka kwake ni kumtolea kisasi, kwa kuwa kupigwa kwa kiungo cha mwenye kuuliwa humpelekea muuwaji kuungama, na mara nyingi kumwona tu aliye uwawa humpelekea mwenye kuuwa kuungama. Na inakuwa kisa hichi ni mbali na lile jambo la kuchinja, na kuamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kuchinja; na kwamba kuamrisha Mwenyezi Mungu Mtukufu wamchinje Ngombe ni kwa ajili ya kumla. Na katika haya pana mafunzo ya nafsi kwao, kwani hawa walikuwa pamoja na Wamisri ambao wakimwona Ngombe ni mtakatifu, na yalikuwa kwao mabaki ya haya ya kumtukuza Ngombe kwa dalili ya kuwa waliabudu sanamu la ndama baada ya hayo. Ikawa hapana budi kungoa mabaki yake katika nafsi zao kwa kuwalazimisha kumchinja Ngombe. Ndio ikawa ile amri ya kuchinja, na yakatokea majadiliano na kukawa kule kusitasita kwao, na mwisho wakamchinja, na walikaribia wasichinje.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Isipo kuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa.
- Nyinyi na baba zenu wa zamani?
- Na unijaalie katika warithi wa Bustani za neema.
- Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika
- Ole wake kila safihi, msengenyaji!
- Na wanapo ambiwa: Kateremsha nini Mola wenu Mlezi? Husema: Hadithi za kubuni za watu wa
- Enyi mlio amini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Mwenyezi Mungu, ili
- Haiwi kuwa makafiri ndio waamirishe misikiti ya Mwenyezi Mungu, hali wanajishuhudishia wenyewe ukafiri. Hao ndio
- Na tulipo chukua ahadi yenu na tukauinua mlima juu yenu (tukakwambieni): Kamateni kwa nguvu haya
- Mwenyezi Mungu aliwaandalia adhabu kali. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, enyi wenye akili, mlio amini! Hakika
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Baqarah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Baqarah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Baqarah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers