Surah Nahl aya 79 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ مُسَخَّرَاتٍ فِي جَوِّ السَّمَاءِ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا اللَّهُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ﴾
[ النحل: 79]
Je! Hawawaoni ndege walivyo wat'iifu katika anga la mbingu? Hapana mwenye kuwashika isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Hakika katika haya zipo ishara kwa watu wanao amini.
Surah An-Nahl in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Do they not see the birds controlled in the atmosphere of the sky? None holds them up except Allah. Indeed in that are signs for a people who believe.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Je! Hawawaoni ndege walivyo watiifu katika anga la mbingu? Hapana mwenye kuwashika isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Hakika katika haya zipo ishara kwa watu wanao amini.
Je! Hao washirikina hawawaangalii ndege walio jaaliwa waweze kuruka hewani juu, kwa kupewa na Mwenyezi Mungu mbawa kubwa kuliko miili yao, wakiikunjua na kuikunja. Na Mwenyezi Mungu akaidhalilisha hewa kuwabeba hao ndege. Hapana anaye washika huko angani ila Mwenyezi Mungu kwa nidhamu aliyo itengeneza Yeye Mwenyewe! Hakika katika kuwatazama hao ndege, na kuzingatia hikima ya Mwenyezi Mungu katika kuwaumba, ni ishara kubwa ya kuwanafiisha walio kuwa tayari kuamini. Ndege wanaruka kwa sababu kadhaa wa kadhaa katika kuumbwa kwao. Muhimu kuliko yote ni lile umbo lao la kuchongoka, na kuwa mbawa zao zilivyo tanda zenye manyoya, na mafupa yenye uwazi na myepesi na vifuko vya hewa kati ya matumbo yao, navyo vimeambatishwa na mayavuyavu (mapafu). Hivyo vifuko hujaa hewa wakati wa kuruka, basi huzidi hao ndege kuwa wepesi.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Isipo kuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na walio sujudu.
- Mola wetu Mlezi! Tulizidiwa na uovu wetu na tukawa watu tulio potea.
- Wawekeni humo humo mnamo kaa nyinyi kwa kadiri ya pato lenu, wala msiwaletee madhara kwa
- Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
- Mwenyezi Mungu amewaahidi wanaafiki wanaume na wanaafiki wanawake na makafiri Moto wa Jahannamu kudumu humo.
- Na kilipo wajia Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha waliyo nayo - na wao
- Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu.
- Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni na hoja wazi.
- Na kwa Haki tumeiteremsha, na kwa Haki imeteremka. Na hatukukutuma ila uwe mbashiri na mwonyaji.
- Naapa kwa mbingu yenye marejeo!
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Nahl with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Nahl mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Nahl Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



