Surah Yusuf aya 83 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿قَالَ بَلْ سَوَّلَتْ لَكُمْ أَنفُسُكُمْ أَمْرًا ۖ فَصَبْرٌ جَمِيلٌ ۖ عَسَى اللَّهُ أَن يَأْتِيَنِي بِهِمْ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُ هُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ﴾
[ يوسف: 83]
Akasema: Bali nafsi zenu zimekushawishini kwenye jambo fulani. Subira ni njema! Asaa Mwenyezi Mungu akaniletea wote pamoja. Hakika Yeye ni Mjuzi Mwenye hikima.
Surah Yusuf in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
[Jacob] said, "Rather, your souls have enticed you to something, so patience is most fitting. Perhaps Allah will bring them to me all together. Indeed it is He who is the Knowing, the Wise."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Akasema: Bali nafsi zenu zimekushawishini kwenye jambo fulani. Subira ni njema! Asaa Mwenyezi Mungu akaniletea wote pamoja. Hakika Yeye ni Mjuzi Mwenye hikima.
Wakarejea wana walio baki kwa Yaaqub. Wakamueleza kama alivyo wausia kaka yao mkubwa. Khabari ile ikamtibua huzuni zake, zikazidi kwa kumpoteza mwanawe wa pili. Wala hakutua nafsi yake kwa kuwa wao hawana makosa ya kusabibisha kupotea kwake, naye angali na machungu kwa waliyo mfanyia Yusuf. Akapiga ukelele kwa kuwatuhumu akiwaambia: Niya yenu haikusalimika katika kumhifadhi mwanangu, lakini nafsi zenu zimekuchocheeni mumpoteze kama mlivyo mpoteza nduguye. Lau kuwa nyinyi hamkutoa fatwa ya kuwa mwizi ashikwe afanywe mtumwa kuwa ndiyo adabu ya mwizi huyo Mheshimiwa asingeli mshika mwanangu, wala asingeli baki kaka yenu huko Misri. Lakini mimi sina hila ila kustahamili katika msiba wangu kwa maliwaza mema, huku nikitaraji kwa Mwenyezi Mungu anirudishie wanangu wote. Kwani Yeye ndiye Mwenye ujuzi ulio zunguka hali yangu na hali zao. Na Yeye ndiye Mwenye hikima yenye kushinda, na kwa hiyo ndio hunitendea na hunipangia.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na wako miongoni mwao wasio jua kusoma; hawakijui Kitabu isipo kuwa uwongo wanao utamani, nao
- Nawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli.
- Tutakuhisabuni enyi makundi mawili.
- Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema.
- Hakika walio amini na wakatenda mema watakuwa nazo Bustani za neema.
- Na walio zikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu na kukutana naye, hao ndio wenye kukata tamaa
- Enyi mlio amini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mcheni Mwenyezi Mungu.
- Wanao toa mali zao kwa Njia ya Mwenyezi Mungu, kisha hawafuatishii masimbulizi wala udhia kwa
- Namna hivi anakubainishieni Mwenyezi Mungu Aya zake ili mpate kufahamu.
- Hakika Qaruni alikuwa katika watu wa Musa, lakini aliwafanyia dhulma. Na tulimpa khazina ambazo funguo
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Yusuf with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Yusuf mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Yusuf Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers