La sourate Al-Mursalat en Swahili
وَالْمُرْسَلَاتِ عُرْفًا(1) Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole! |
فَالْعَاصِفَاتِ عَصْفًا(2) Na zinazo vuma kwa kasi! |
وَالنَّاشِرَاتِ نَشْرًا(3) Na zikaeneza maeneo yote! |
فَالْفَارِقَاتِ فَرْقًا(4) Na zinazo farikisha zikatawanya! |
فَالْمُلْقِيَاتِ ذِكْرًا(5) Na zinazo peleka mawaidha! |
عُذْرًا أَوْ نُذْرًا(6) Kwa kuudhuru au kuonya, |
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَاقِعٌ(7) Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa! |
فَإِذَا النُّجُومُ طُمِسَتْ(8) Wakati nyota zitakapo futwa, |
وَإِذَا السَّمَاءُ فُرِجَتْ(9) Na mbingu zitakapo pasuliwa, |
وَإِذَا الْجِبَالُ نُسِفَتْ(10) Na milima itakapo peperushwa, |
وَإِذَا الرُّسُلُ أُقِّتَتْ(11) Na Mitume watakapo wekewa wakati wao, |
لِأَيِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ(12) Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo? |
لِيَوْمِ الْفَصْلِ(13) Kwa siku ya kupambanua! |
وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الْفَصْلِ(14) Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini? |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ(15) Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha! |
أَلَمْ نُهْلِكِ الْأَوَّلِينَ(16) Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia? |
ثُمَّ نُتْبِعُهُمُ الْآخِرِينَ(17) Kisha tukawafuatilizia walio fuatia? |
كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ(18) Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu! |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ(19) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّاءٍ مَّهِينٍ(20) Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa? |
فَجَعَلْنَاهُ فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ(21) Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti? |
إِلَىٰ قَدَرٍ مَّعْلُومٍ(22) Mpaka muda maalumu? |
فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ الْقَادِرُونَ(23) Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria. |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ(24) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ كِفَاتًا(25) Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya |
أَحْيَاءً وَأَمْوَاتًا(26) Walio hai na maiti? |
وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ شَامِخَاتٍ وَأَسْقَيْنَاكُم مَّاءً فُرَاتًا(27) Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu? |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ(28) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
انطَلِقُوا إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ(29) Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha! |
انطَلِقُوا إِلَىٰ ظِلٍّ ذِي ثَلَاثِ شُعَبٍ(30) Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu! |
لَّا ظَلِيلٍ وَلَا يُغْنِي مِنَ اللَّهَبِ(31) Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako. |
إِنَّهَا تَرْمِي بِشَرَرٍ كَالْقَصْرِ(32) Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba! |
كَأَنَّهُ جِمَالَتٌ صُفْرٌ(33) Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano! |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ(34) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
هَٰذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ(35) Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu, |
وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ(36) Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru. |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ(37) Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! |
هَٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ ۖ جَمَعْنَاكُمْ وَالْأَوَّلِينَ(38) Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia. |
فَإِن كَانَ لَكُمْ كَيْدٌ فَكِيدُونِ(39) Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi! |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ(40) Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! |
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلَالٍ وَعُيُونٍ(41) Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem, |
وَفَوَاكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ(42) Na matunda wanayo yapenda, |
كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ(43) Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda. |
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ(44) Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema. |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ(45) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
كُلُوا وَتَمَتَّعُوا قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجْرِمُونَ(46) Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu! |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ(47) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ارْكَعُوا لَا يَرْكَعُونَ(48) Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami. |
وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ(49) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ(50) Basi maneno gani baada ya haya watayaamini? |
Plus de sourates en Swahili :
Téléchargez la sourate avec la voix des récitants du Coran les plus célèbres :
Téléchargez le fichier mp3 de la sourate Al-Mursalat : choisissez le récitateur pour écouter et télécharger la sourate Al-Mursalat complète en haute qualité.















Donnez-nous une invitation valide