Surah Anfal aya 1 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّهِ وَالرَّسُولِ ۖ فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ﴾
[ الأنفال: 1]
Wanakuuliza juu ya Ngawira. Sema: Ngawira ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na suluhisheni mambo baina yenu, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini.
Surah Al-Anfal in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
They ask you, [O Muhammad], about the bounties [of war]. Say, "The [decision concerning] bounties is for Allah and the Messenger." So fear Allah and amend that which is between you and obey Allah and His Messenger, if you should be believers.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Wanakuuliza juu ya Ngawira. Sema: Ngawira ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na suluhisheni mambo baina yenu, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini.
Nabii Muhammad (s.a.w.) katolewa Makka na kalazimishwa kuihama kwa sababu ya vitimbi vya mapagani, washirikina, na kwa kuazimia kwao kumuuwa, ili Waislamu wapate kuwa na dola yao. Naye akenda kukaa Madina kwenye amani na manusura. Huko ikawa hapana budi ila kuwania kujilinda na uvamizi wa maadui, wasije wenye Imani wakapata mateso. Vikatokea hivyo Vita vya Badri. Waumini wakapata ushindi ulio wazi na ngawira nyingi waliziteka. Ikatokea khitilafu kidogo na suala katika shauri la ugawaji wa hizo ngawira. Ndio hivyo Mwenyezi Mungu anasema: Wanakuuliza khabari ya ngawira, zende wapi? Apewe nani? Ni za nani? Zigawanywe vipi? Ewe Nabii! Waambie: Hizo ngawira ni za Mwenyezi Mungu kwanza. Na Mtume, kwa amri ya Mola wake Mlezi, ndiye mwenye madaraka ya kuzigawa. Basi wacheni kukhitalifiana kwa ajili ya hayo. Na uwe mtindo wenu ni kumkhofu Mwenyezi Mungu na kumtii. Na tengenezeni yaliyo baina yenu, na mfanye mapenzi na uadilifu ndio makhusiano baina yenu. Kwani hakika hizi ndizo sifa za watu wa Imani.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Je! Huu ni uchawi, au hamwoni tu?
- Laiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa.
- Wala msimuamini ila anaye fuata dini yenu. Sema: Hakika uwongofu ni uwongofu wa Mwenyezi Mungu,
- Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.
- Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na anaye fanya hivyo, basi hatakuwa
- Au uwe na kitalu cha mitende na mizabibu, na utupitishie mito kati yake ikimiminika.
- Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Wala wao
- Na tukamuandikia katika mbao kila kitu, mawaidha na maelezo ya mambo yote. (Tukamwambia): Basi yashike
- Kumbuka alipo kuonyesha usingizini mwako kwamba wao ni wachache - na lau angeli kuonyesha kuwa
- Na akasema yule aliye amini: Enyi watu wangu! Hakika mimi nakukhofieni mfano wa siku za
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anfal with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anfal mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anfal Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers