Surah Anam aya 100 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَجَعَلُوا لِلَّهِ شُرَكَاءَ الْجِنَّ وَخَلَقَهُمْ ۖ وَخَرَقُوا لَهُ بَنِينَ وَبَنَاتٍ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ﴾
[ الأنعام: 100]
Bado wamemfanyia Mwenyezi Mungu majini kuwa washirika wake, na hali Yeye ndiye aliye waumba. Na wakamzulia, bila ya ujuzi wowote, kuwa ana wana wa kiume na wa kike. Subhanahu, Ametakasika na ametukuka juu ya hayo wanayo mbandikiza nayo!
Surah Al-Anam in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
But they have attributed to Allah partners - the jinn, while He has created them - and have fabricated for Him sons and daughters. Exalted is He and high above what they describe
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Bado wamemfanyia Mwenyezi Mungu majini kuwa washirika wake, na hali Yeye ndiye aliye waumba. Na wakamzulia, bila ya ujuzi wowote, kuwa ana wana wa kiume na wa kike. Subhanahu, Ametakasika na ametukuka juu ya hayo wanayo mbandikiza nayo!.
Juu ya dalili hizi makafiri wamewafanya Malaika na mashetani ni washirika wa Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ndiye aliye waumba hao. Haiwafalii kujua hayo wakamuabudu asiye kuwa Yeye, naye ndiye aliye waumba Malaika na mashetani. Haitakikani wawaabudu hao nao wameumbwa kama wao!! Na hawa makafiri wakambunia Mwenyezi Mungu wana. Wakristo wakadai kuwa Masihi ni mwana wa Mungu, na baadhi ya washirikina wa Kiarabu wakadai kuwa Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu. Na huo ni ujinga, kutokuwa na ilimu! Mwenyezi Mungu Mtukufu ameepukana na hayo wanayo muambatisha naye Subhana!
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na wanasema: Lini ahadi hii, ikiwa mnasema kweli?
- Na ikiwa mkateleza baada ya kukufikieni hoja zilizo wazi, basi jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni
- Na wapeni mayatima mali yao. Wala msibadilishe kibaya kwa kizuri. Wala msile mali zao pamoja
- Nao, badala ya Mwenyezi Mungu, wanaabudu wasio wadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema: Hawa ndio waombezi
- Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
- Na kwa ardhi inayo pasuka!
- Firauni akawafuata pamoja na majeshi yake. Basi kiliwafudikiza humo baharini kilicho wafudikiza.
- Wakasema: Ee baba yetu! Tuombee msamaha kwa dhambi zetu. Hapana shaka sisi tulikuwa na makosa.
- Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia?
- Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ila kwa ajili ya Haki. Na
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anam with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anam mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anam Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers