Surah Tawbah aya 107 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مَسْجِدًا ضِرَارًا وَكُفْرًا وَتَفْرِيقًا بَيْنَ الْمُؤْمِنِينَ وَإِرْصَادًا لِّمَنْ حَارَبَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ مِن قَبْلُ ۚ وَلَيَحْلِفُنَّ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا الْحُسْنَىٰ ۖ وَاللَّهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ﴾
[ التوبة: 107]
Na wapo walio jenga msikiti kwa ajili ya madhara na ukafiri na kuwafarikisha Waumini, na pa kuvizia kwa walio mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake hapo kabla. Na bila ya shaka wataapa kwamba: Hatukukusudia ila wema tu. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa wao ni waongo.
Surah At-Tawbah in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And [there are] those [hypocrites] who took for themselves a mosque for causing harm and disbelief and division among the believers and as a station for whoever had warred against Allah and His Messenger before. And they will surely swear, "We intended only the best." And Allah testifies that indeed they are liars.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na wapo walio jenga msikiti kwa ajili ya madhara na ukafiri na kuwafarikisha Waumini, na pa kuvizia kwa walio mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake hapo kabla. Na bila ya shaka wataapa kwamba: Hatukukusudia ila wema tu. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa wao ni waongo.
Na miongoni mwa wanaafiki walikuwapo jamaa walio jenga msikiti si kwa kutafuta ridhaa ya Mwenyezi Mungu, bali wakikusudia madhara, na kufuru, na kuwagawa Waumini. Na wao wataapa kuwa wao hawakutaka kwa kujenga msikiti huo ila kheri na amali njema. Na Mwenyezi Mungu anawashuhudia kuwa ni waongo katika hiyo Imani yao. Msikiti ulio tajwa katika Aya ulijengwa na baadhi ya wanaafiki wa Madina walio azimia shari. Waliudhika kujengwa Masjid Qubaa walio ujenga Banu Amri bin Auf, na akaubariki Mtume s.a.w. kwa kuswali ndani yake. Basi Ibn Aamir Arrahib (aliye itwa Rahib, Mmonaki, kwa kushirikiana kwake na Mapadri) aliwachochea hao wanaafiki wajenge nao Msikiti wa ushinde kushindana na walio jenga Masjid Qubaa, ili uwepo ushinde wa kijahili kwa kila mmoja kujitapa kwa kujenga msikiti. Vile vile ilikuwa azma yao wafanye hapo ni kioteo pa kukutania siri kupanga njama za kuwadhuru Waumini. Baada ya kwisha jenga walimualika Mtume s.a.w. ende kuswali humo, wafanye hiyo sala ndio ada tena ya ushindani wao na kuwafarikisha Waumini. Mtume alitaka kuitikia wito wao bila ya kujua njama zao. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu alimjuvya alipo kuwa anarudi kutoka vita vya Tabuk na azma yake ya kuitikia wito. Na Yeye Subhanahu akamkataza asisimame kabisa katika msikiti huo, licha ya kuswali ndani yake.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Hawangojei ila ukelele mmoja tu utakao wachukua nao wamo kuzozana.
- Iwe salama kwa Ilyas.
- Je! Hujui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo mbinguni na katika ardhi? Hakika hayo yamo Kitabuni.
- Ati aliye lelewa katika mapambo, na katika mabishano hawezi kusema kwa bayana...?
- Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu.
- Hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika duniani na Akhera. Nao hawatapata wa kuwanusuru.
- Na Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa watu wawili. Mmoja wao ni bubu, hawezi chochote, naye
- Hakika walio kufuru lau wange kuwa na yote yaliyomo duniani, na mengine kama hayo, ili
- Hakika wale walio zikataa Ishara zetu tutawaingiza Motoni. Kila zitapo wiva ngozi zao tutawabadilishia ngozi
- Au mnayo hoja iliyo wazi?
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Tawbah with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Tawbah mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Tawbah Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



