Surah Hud aya 12 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿فَلَعَلَّكَ تَارِكٌ بَعْضَ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ وَضَائِقٌ بِهِ صَدْرُكَ أَن يَقُولُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ كَنزٌ أَوْ جَاءَ مَعَهُ مَلَكٌ ۚ إِنَّمَا أَنتَ نَذِيرٌ ۚ وَاللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ﴾
[ هود: 12]
Basi labda utaacha baadhi ya yale yaliyo funuliwa kwako, na kifua kitaona dhiki kwa hayo, kwa sababu wanasema: Mbona hakuteremshiwa khazina, au wakaja naye Malaika? Wewe ni mwonyaji tu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa kila kitu.
Surah Hud in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Then would you possibly leave [out] some of what is revealed to you, or is your breast constrained by it because they say, "Why has there not been sent down to him a treasure or come with him an angel?" But you are only a warner. And Allah is Disposer of all things.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Basi labda utaacha baadhi ya yale yaliyo funuliwa kwako, na kifua kitaona dhiki kwa hayo, kwa sababu wanasema: Mbona hakuteremshiwa khazina, au wakaja naye Malaika? Wewe ni mwonyaji tu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa kila kitu.
Ewe Nabii! Usijaribu kutaka kuwaridhi washirikina, kwani hao hawaamini. Na huenda ukijaribu kutaka kuwaridhi ukaacha kusoma baadhi ya uliyo letewa Wahyi, katika yale wasiyo penda wao kuyasikia, kama vile kudharauliwa baadhi ya miungu yao, kwa kukhofu kuwa wasije wakakejeli! Na huenda pengine ukahisi dhiki unapo wasomea, kwa kuwa wao wanataka Mwenyezi Mungu akuteremshie khazina ustarehe nayo kama wafalme, au waje nawe malaika watwambie ukweli wake! Basi, ewe Nabii! Usizibali inadi zao. Kwani wewe si chochote ila ni mwonyaji na mhadharishaji wa adhabu za Mwenyezi Mungu kwa anaye kwenda kinyume na amri yake. Nawe hayo umefanya, basi jipumzishe nafsi yako nao. Na jua kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuangalia na kulinda kila kitu. Naye atawafanyia kama wanavyo stahiki.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na hakika walikwisha muahidi Mwenyezi Mungu kabla yake kwamba hawatageuza migongo yao. Na ahadi ya
- Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili?
- Vikaifunika vilivyo funika.
- Mataifa mangapi tumeyaangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa kuokoka ulikwisha pita.
- Na siku watakapo letwa walio kufuru kwenye Moto wataambiwa: Nyinyi mlitwaa vitu vyenu vizuri katika
- Na mkewe alikuwa kasimama wima, akacheka. Basi tukambashiria (kuzaliwa) Is-haq, na baada ya Is-haq Yaaqub.
- (Malkia) akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika nimeletewa barua tukufu.
- Zilizo inuliwa, zilizo takaswa.
- Tena la! Karibu watakuja jua.
- Wakasema: Ewe Shua'ibu! Mengi katika hayo unayo yasema hatuyafahamu. Na sisi tunakuona huna nguvu kwetu.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Hud with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Hud mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Hud Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers