Surah Hud aya 13 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِعَشْرِ سُوَرٍ مِّثْلِهِ مُفْتَرَيَاتٍ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللَّهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴾
[ هود: 13]
Au wanasema: Ameizua? Sema: Basi leteni Sura kumi zilizo zuliwa mfano wa hii, na waiteni muwawezao badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli.
Surah Hud in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
Or do they say, "He invented it"? Say, "Then bring ten surahs like it that have been invented and call upon [for assistance] whomever you can besides Allah, if you should be truthful."
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Au wanasema: Ameizua? Sema: Basi leteni Sura kumi zilizo zuliwa mfano wa hii, na waiteni muwawezao badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli.
Katika Qurani ipo Ishara inayo thibitisha ukweli wako. Basi wao wakisema, kuwa hii umeitunga wewe na umemzulia Mwenyezi Mungu, wewe waambie: Ikiwa Qurani hii imetokana na mwanaadamu, basi yamkinika mwanaadamu mwengine kuleta mfano wake. Na nyinyi ni mafasihi kuliko wote. Basi leteni Sura kumi kama hii mbali mbali, na mtakeni msaada yeyote mnaye weza kumtaka, katika watu na majini, kama hakika mnasema kweli katika hayo madai yenu kuwa haya ni maneno ya binaadamu. Qurani si muujiza tu katika maandishi yake, bali ndani yake mna hadithi za kweli, na ilimu mbali mbali za sayansi za uumbaji zilizo ashiriwa, na hazikuwa zikijuulikana wakati wa kuteremka kwake, na pia katika hukumu ziliomo ndani yake.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Basi Shet'ani aliwatia wasiwasi ili kuwafichulia tupu zao walizo fichiwa, na akasema: Mola Mlezi wenu
- Na pindi tukitaka kuuteketeza mji huwaamrisha wale wenye starehe na taanusi, lakini wao huendelea kutenda
- Na walisema: Nyoyo zetu zimefunikwa. Bali Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufuru zao: kwa hivyo ni
- Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu.
- Wakasema: Nani aliye ifanyia haya miungu yetu? Hakika huyu ni katika walio dhulumu.
- Akasema: Hakika mimi nachelea wasinikanushe.
- Siku ambayo hautawafaa madhaalimu udhuru wao, nao watapata laana, na watapata makaazi mabaya kabisa.
- Bali wanaikanusha Saa (ya Kiyama). Na Sisi tumemuandalia Moto mkali kabisa huyo mwenye kuikanusha Saa..
- Mwenyezi Mungu amemlaani. Naye Shet'ani alisema: Kwa yakini nitawachukua sehemu maalumu katika waja wako.
- Yasikufurahishe mali yao wala wana wao. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaadhibu kwayo hapa duniani, na
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Hud with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Hud mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Hud Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers