Surah Yunus aya 24 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿إِنَّمَا مَثَلُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ مِمَّا يَأْكُلُ النَّاسُ وَالْأَنْعَامُ حَتَّىٰ إِذَا أَخَذَتِ الْأَرْضُ زُخْرُفَهَا وَازَّيَّنَتْ وَظَنَّ أَهْلُهَا أَنَّهُمْ قَادِرُونَ عَلَيْهَا أَتَاهَا أَمْرُنَا لَيْلًا أَوْ نَهَارًا فَجَعَلْنَاهَا حَصِيدًا كَأَن لَّمْ تَغْنَ بِالْأَمْسِ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ﴾
[ يونس: 24]
Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama maji tuliyo yateremsha kutoka mbinguni, kisha yakachanganyika na mimea ya ardhi wanayo ila watu na wanyama. Mpaka ardhi ilipo kamilika uzuri wake, na ikapambika, na wenyewe wakadhani wamesha iweza, iliifikia amri yetu usiku au mchana, tukaifanya kama iliyo fyekwa - kama kwamba haikuwapo jana. Namna hivi tunazipambanua Ishara zetu kwa watu wanao fikiri.
Surah Yunus in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
The example of [this] worldly life is but like rain which We have sent down from the sky that the plants of the earth absorb - [those] from which men and livestock eat - until, when the earth has taken on its adornment and is beautified and its people suppose that they have capability over it, there comes to it Our command by night or by day, and We make it as a harvest, as if it had not flourished yesterday. Thus do We explain in detail the signs for a people who give thought.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama maji tuliyo yateremsha kutoka mbinguni, kisha yakachanganyika na mimea ya ardhi wanayo ila watu na wanyama. Mpaka ardhi ilipo kamilika uzuri wake, na ikapambika, na wenyewe wakadhani wamesha iweza, iliifikia amri yetu usiku au mchana, tukaifanya kama iliyo fyekwa - kama kwamba haikuwapo jana. Namna hivi tunazipambanua Ishara zetu kwa watu wanao fikiri.
Hakika hali ya uhai wa dunia kwa uzuri wake na starehe zake, na kisha baada ya hayo kutoweka, si chochote ila ni kama hali ya maji yanayo teremka mbinguni, yakachanganyika na mimea ya ardhi inayo liwa na watu na wanyama. Mimea hiyo ikastawi na ikatoa matunda, na ardhi ikapambika kwa kunawiri. Uzuri huo ukisha fika ukomo wake, na wenyewe wakayakinika kuwa kweli ni mali yao, na kuwa watanafiika kwa matunda yake na neema zake, amri yetu ya kuondoa yote hayo ikaja. Tukaifanya kama kwamba iliyo fyekwa, na kama kwamba haijapata kukaliwa wala haikupata kuwa na uzuri kabla yake! Na hali zote mbili za kustawi na kunawiri ya kufurahia watu na kinyume cha hayo, ni mambo ya kuondoka na kutoweka! Na kama alivyo bainisha Mwenyezi Mungu kwa mifano iliyo wazi, anabainisha Aya zake na anafafanua hukumu zake na Ishara kwa watu wanao fikiri na wanapima kwa akili. Aya hii inaashiria ukweli ulio anza kuchomoza, nao ni kuwa mwanaadamu kwa kuifanya ilimu imtumikie ameweza kuyamiliki anayo yataka. Hata inapo kuwa karibu ya kufikilia ukweli huu kukamilika, na akaona huyo mwanaadamu amekwisha fikilia kilele cha ujuzi, hapo basi amri ya Mwenyezi Mungu hutokea.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye,
- Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na tafuteni njia ya kumfikilia. Na wanieni kwa juhudi
- Na lau kuwa tumewaamrisha: Jiueni, au tokeni majumbani kwenu, wasingeli fanya hayo ila wachache tu
- Ukafika msafara, wakamtuma mchota maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake. Alisema: Kheri Inshallah! Huyu hapa
- Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua!
- Kwa yakini tukiona unavyo geuza geuza uso wako mbinguni. Basi tutakuelekeza kwenye Kibla ukipendacho. Basi
- Ambao husikiliza maneno, wakafuata lilio bora yao. Hao ndio alio waongoa Mwenyezi Mungu, na hao
- Bustani za milele zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na hayo ni malipo ya mwenye
- KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.
- Enyi mlio amini! Chukueni hadhari yenu! Na mtoke kwa vikosi au tokeni nyote pamoja!
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Yunus with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Yunus mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Yunus Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers