Surah Anbiya aya 31 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَجَعَلْنَا فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِهِمْ وَجَعَلْنَا فِيهَا فِجَاجًا سُبُلًا لَّعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ﴾
[ الأنبياء: 31]
Na tukaweka katika ardhi milima iliyo thibiti ili isiwayumbishe, na tukaweka humo njia pana ili wapate kuongoka.
Surah Al-Anbiya in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And We placed within the earth firmly set mountains, lest it should shift with them, and We made therein [mountain] passes [as] roads that they might be guided.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na tukaweka katika ardhi milima iliyo thibiti ili isiwayumbishe, na tukaweka humo njia pana ili wapate kuongoka.
Na katika dalili za uweza wetu ni kuwa tumeifanya milima imesimama imara kwenye ardhi ili isiyumbeyumbe nao watu, na tumefanya humo njia pana, za kupitia kwa wasaa, ili waweze kuongoza njia humo kwa makusudio yao. Maoni ya wataalamu juu ya Aya ya 31: -Na tukaweka katika ardhi milima iliyo thibiti ili isiwayumbishe, na tukaweka humo njia pana ili wapate kuongoka.- Ilivyo kuwa ndani ya ardhi kila kitu kimeyayuka, na lau kuwa milima imewekwa tu katika baadhi ya sehemu za huu mpira wa dunia kama majabali yaliyo nyanyuka juu tu, uzito wao ungeli sabibisha gamba la dunia liyumbe, au lipindane na kupasuka. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu kwa utukufu wa shani yake ameifanya milima isimame imara kwa kuwa na mizizi iliyo zama kwenye gamba la ardhi mpaka chini kwenye kina kirefu kulingana na urefu wake kwendea juu. Kwa hivyo imekuwa hiyo milima kama vigingi, kama alivyo jaalia eneo la minyanyuka hii na mizizi ni duni kuliko maeneo ya gamba lilio zunguka. Yote haya ni kwa ajili ya kueneza sawa uzito wa juu ya gamba kwa pande zote ili pasiwepo kuyumbayumba na kupasuka. Kwani hakika kuenezwa kwa uzito juu ya uso wa dunia yakaribia kuwa hakuleti athari kubwa ya kutajika. Na ilimu za kisasa zimethibitisha kuwa kuenezwa kwa nchi kavu na maji juu ya ardhi, na kuwepo mfululizo wa milima juu yake ni katika yanayo hakikisha hali ilivyo ardhi, na imethibitika kuwa chini ya milima mizito kuna vitu vyepesi kubungunyika, na chini ya maji ya bahari kuu vipo vitu vizito. Kwa kuenezwa uzani wa namna hiyo mbali mbali katika dunia, na mgawanyo huu wa milima, makusudio yake ni kusawizisha uzani wa mpira huu wa ardhi. Na ilivyo nyanyuka milima zikatokea nyanda na mabonde na njia baina ya milima na mwambao na bahari na minyanyuko, na zikawa njia.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Na uchochezi wa Shet'ani ukikuchochea basi omba ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Msikizi,
- Na wanao jitetea baada ya kudhulumiwa, hao hapana njia ya kuwalaumu.
- Na wale ambao Ishara za Mola wao Mlezi wanaziamini,
- Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika nchi kwa maringo. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila anaye
- Na siku zitapo funguka mbingu kwa mawingu, na wateremshwe Malaika kwa wingi,
- Kisha itakuja baadaye miaka saba ya shida itakayo kula kile mlicho iwekea isipo kuwa kidogo
- Shetani amewatawala na akawasahaulisha kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hao ndio kundi la Shetani. Kweli hakika kundi
- Na amani iwe juu yake siku ya kuzaliwa, na siku ya kufa, na siku ya
- Au wao wanao miungu watao weza kuwakinga nasi? Hao hawawezi kujinusuru nafsi zao, wala hawatalindwa
- Naye ndiye aliye muumba mwanaadamu kutokana na maji, akamjaalia kuwa na nasaba na ushemeji. Na
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anbiya with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anbiya mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anbiya Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers