Surah Anbiya aya 32 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَجَعَلْنَا السَّمَاءَ سَقْفًا مَّحْفُوظًا ۖ وَهُمْ عَنْ آيَاتِهَا مُعْرِضُونَ﴾
[ الأنبياء: 32]
Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyo hifadhiwa, lakini wanazipuuza Ishara zake.
Surah Al-Anbiya in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
And We made the sky a protected ceiling, but they, from its signs, are turning away.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyo hifadhiwa, lakini wanazipuuza Ishara zake.
Na tumeifanya mbingu kama dari iliyo nyanyuliwa, na tukailinda isianguke, au visianguke viliomo humo. Na juu ya hayo, wao hawazioni wala hawaziingatii Ishara zetu zenye kuonyesha uweza wetu na hikima yetu na rehema yetu. Maoni ya wataalamu juu ya Aya 32: -Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyo hifadhiwa lakini wanazipuuza Ishara zake. -: Aya hii tukufu imethibitisha kuwa mbingu na vyote viliomo ndani yake vimehifadhiwa visiwe na ila yoyote, na vimehifadhiwa visidondoke juu ya ardhi. Na mbingu ni kila kilicho juu yetu, kuanzia kifuniko hichi cha hewa inayo walinda walioko juu ya ardhi na khatari nyingi za angani ambazo zinazuia maisha, mfano wa vimondo vya nyota za mkia, na miyale. Na juu ya ardhi pana kifuniko cha hewa kinacho linda ardhi kwa nguvu za mvutano, na haifai kukosekana hivyo bila ya maangamizo kabisa. Na juu ya kifuniko cha hewa ndio kuna hizo sayari za mbinguni, na zipo kwa umbali mbali mbali kufuatana na nyendo zao tangu mwanzo. -Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyo hifadhiwa- yaani hizo sayari na vyote vilio mbinguni vyaonekana kwa nadhari yetu kama kwamba ni dari, na tunaona vilio juu ya vichwa vyetu kama ni vidogo kuliko vilioko upeo wa macho. Na hayo ni kiini macho tu, kama tunapo liona jua kubwa wakati wa kuchomoza na kuchwa kuliko adhuhuri. Na hili qubba la mbingu lina sifa zake, zinazo khitalifiana kila ukizidi mnyanyuko wa ardhi, kama hizo sayari za mbinguni kwa mujibu wa jicho linavyo ona katika qubba la mbingu.
English | Türkçe | Indonesia |
Русский | Français | فارسی |
تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.
- Isipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
- Nasi tutaweka mizani za uadilifu kwa Siku ya Kiyama. Basi nafsi haitadhulumiwa kitu chochote. Hata
- Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtu mwenye mabwana washirika wanao gombana, na wa mtu mwengine
- Ametukuka ambaye akitaka atakujaalia yaliyo bora kuliko hayo, nayo ni mabustani yapitayo mito kati yao,
- Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki
- Je! Huu ni uchawi, au hamwoni tu?
- Wala hawakusema: Mungu akipenda!
- Na akakanusha lilio jema,
- Kila khabari ina kipindi chake. Nanyi mtakuja jua.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anbiya with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anbiya mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anbiya Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Abdul Rashid Sufi
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers