Surah Anfal aya 34 , Swahili translation of the meaning Ayah.
﴿وَمَا لَهُمْ أَلَّا يُعَذِّبَهُمُ اللَّهُ وَهُمْ يَصُدُّونَ عَنِ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَمَا كَانُوا أَوْلِيَاءَهُ ۚ إِنْ أَوْلِيَاؤُهُ إِلَّا الْمُتَّقُونَ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ﴾
[ الأنفال: 34]
Lakini wana jambo gani hata Mwenyezi Mungu asiwaadhibu, na hali ya kuwa wanawazuilia watu Msikiti Mtakatifu? Wala wao hawakuwa ndio walinzi wake, bali walinzi wake hawakuwa ila wacha-Mngu tu. Lakini wengi katika wao hawajui.
Surah Al-Anfal in SwahiliSwahili Translation - Al-Barwani
English - Sahih International
But why should Allah not punish them while they obstruct [people] from al-Masjid al- Haram and they were not [fit to be] its guardians? Its [true] guardians are not but the righteous, but most of them do not know.
Tafsiri ya maana yake kwenye lugha ya Kiswahili
Lakini wana jambo gani hata Mwenyezi Mungu asiwaadhibu, na hali ya kuwa wanawazuilia watu Msikiti Mtakatifu? Wala wao hawakuwa ndio walinzi wake, bali walinzi wake hawakuwa ila wacha-Mngu tu. Lakini wengi katika wao hawajui.
Hakika hali yao iliyo sasa inaruhusu kuwaadhibu, kwani wanawazuia watu wasiutumie Msikiti ambao Mwenyezi Mungu ameutukuza kwa kuharimisha vita karibu yake. Lakini Mwenyezi Mungu anawaakhirisha kwa alivyo wakadiria katika ujuzi wake kuwa wengi wao watakuja amini. Wao wakati huu wa sasa sio walinzi wa kuunusuru huo Msikiti Mtukufu, bali wao wameunajisi kwa kutia ibada ya masanamu ndani yake. Ama wa kuunusuru hakika ni Waumini, wenye kumtii Mwenyezi Mungu. Lakini wengi katika washirikina hawaijui Dini, wala hawajui cheo cha Nyumba hiyo Tukufu.
| English | Türkçe | Indonesia |
| Русский | Français | فارسی |
| تفسير | Bengali | Urdu |
Ayats from Quran in Swahili
- Iwe salama kwa Musa na Haruni!
- Hao ni watu walio kwisha pita. Watapata waliyo yachuma, nanyi mtapata mtakayo yachuma; wala hamtaulizwa
- Wala giza na mwangaza.
- Huu ni Ukumbusho wa rehema ya Mola wako Mlezi kwa mja wake, Zakariya.
- Wataelekeana wakiulizana.
- Na wakasema: Tukiufuata uwongofu huu pamoja nawe tutanyakuliwa kutoka nchi yetu. Je! Kwani Sisi hatukuwaweka
- Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea kwa Mola wa walimwengu
- Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba.
- Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema.
- Enyi mlio amini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mcheni Mwenyezi Mungu.
Quran Surah in Swahili :
Download Surah Anfal with the voice of the most famous Quran reciters :
Surah Anfal mp3 : choose the reciter to listen and download the chapter Anfal Complete with high quality
Ahmed Al Ajmy
Bandar Balila
Khalid Al Jalil
Saad Al Ghamdi
Saud Al Shuraim
Abdul Basit
Ammar Al-Mulla
Abdullah Basfar
Abdullah Al Juhani
Fares Abbad
Maher Al Muaiqly
Al Minshawi
Al Hosary
Mishari Al-afasi
Yasser Al Dosari
Please remember us in your sincere prayers



